Siku moja ina masaa 24. Ndani ya muda huu (yaaniasaa 24) kuna muda wa kulala, kufanya kazi, kutembea kutoka eneo moja kwenda jingine. Muda wote huu ukiuunganisha unapata karibia masaa 20 ambayo yanatumika. Ila cha kufurahisha ni kwamba unabakiza masaa 4 ambayo yapo yapo tu.
Watu wengi huyatumia masaa haya kuangalia tamthiliya, kupiga soga na mambo mengine ambayo hayajengi.
Huu muda unapaswa kuutumia wewe vizuri sana. Na ili uutumie vyema muda huu utapaswa kwenda kinyume na mazoea.
MAZOEA: Ulikuwa unaangalia movie.
MAISHA MAPYA: Achana na kuangali tamthiliya.
MAZOEA: Ulikuwa unazurura kupiga soga.
MAISHA MAPYA: Achana na huyo utartibu
Sasa utajiuliza Je, mbona haiwezekani?
Na Mimi nakwambia kwa nini isiwezekane?
Je, ni kitu gani unafaidika nacho kwa kuangalia tamthiliya? Ni kitu gani?
Hivi unaonaje ykianza kufanya kitu ambacho kinakujenga zaidi wewe?
SWALI: NIKIACHANA NA HIVYO VITU NIFANYE NINI?
Hapa Sasa ndipo tunakuja kwenye mara kuu ya siku ya leo. Tumeona kwamba ukiachana na vitu vyote ambavyo havina maana unaweza kubaki na masaa manne na zaidi. Sasa utumie muda huu kuwekeza katika wewe. Utumie muda huu kusoma vitu ambavyo vunakusogeza mbele zaidi. Utumie muda huu kujifunza ujuzi mpya.
Utumie muda huu kujifunza lugha mpya.
Utumie muda huu kuelewa zaidi eneo lako la kazi kiundani. Hivi ndivyo unaweza kuutumia muda wako vizuri sana kuliko mtu mwingine yeyote.
Soma Zaidi: Ongeza Ufanisi Wako Kwa Kufanya Vitu Vitatu Kila Siku
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391