Huu Ndio Ushauri Ambao Andrew Carnegie Anatoa Kwa Kila Mtu


Andrew Carnegie alikuwa mwanaviwanda wa karne 19 na 20 katika nchi ya Marekani. Kupitia kiwanda chake cha vyuma (steel industry) Carnegie alitengeneza utajiri mkubwa sana. Mpaka Sasa Carnegie ni miongoni mwa matajiri kumi wa nyakati zote.

Kwa mtu kama huyu tuna mengi sana ya kujifunza. Historia yake tu ni somo kubwa. Sasa leo nimekuandalia mambo 9 ya kujifunza kutoka kwake.

1. Kama huwezi kujihamasiha mwenyewe, basi kubali kuwa wa kawaida hata kama una kipaji kikubwa kiasi gani.
Hamasa ni miongoni mwa vitu ambavyo havidumu. Leo hii unaweza kuwa na hamasa kubwa ila kesho hamasa yako ikapotea. Ndio maana mwanzoni mwa mwaka, watu huwa wanakuwa na hamasa kubwa ila kufikia katikati ya mwaka watu hao huwa hawana hamasa tena. Wengine huwa wanapata hamasa mara moja na kujikuta wanaweka  mipango mikubwa ila mwishoni mwa mwaka ndio kabisaa hawakumbuki waliiweka wapi.

Zig Ziglar aliulizwa juu ya hili suala la hamasa kupanda kwa muda mfupi baadae kumalengo naye alikuwa na haya ya kusema, “hamasa ni kama kuoga. Hauogi mara moja tu na kuacha. Unaoga kila siku”
Kumbe na hamasa tunaihitaji kila siku na tunapaswa kuitafuta kila siku. Je, unafanya nini kujihamasisha?
Ndio maana Andrew Carnegie anatutaka tujihamasishe ili tufanikiwe zaidi.

Soma Zaidi; When One Plus One R
Does Not Become Two

2. Watu waliofanikiwa ni wale ambao wamechagua kitu kimoja na wanafanya hicho.

Hivi kwa mfano likitajwa jina lako ni kitu gani kimoja tunaweza kuongea juu yako?
Ukifuatilia watu wengi wenye mafanikio makubwa utagundua kwamba watu hawa ni wale ambao wamechagua kitu kimoja katika maisha yao na wao kazi yao ni kuwa bora katika hicho.
Ukiongea juu ya Michael Jordan unaongelea mpira wa kikapu (basketball).
Ukiongelea huu ya Michael Jackson basi ni mziki.
Ukiongea juu ya Mohammed Ali basi ni masumbwi.
Ukiongelewa wewe je?

3. Siri ya mafanikio sio kufanya kila kitu wewe. Bali ni kugundua watu sahihi wa kukusaidia kukifanya.

Kama umewahi kufuatilia watu ambao wamefanya makubwa kwenye uwanja wa biashara sio wale ambao wanafanya kazi peke yao. Bali wale ambao wanaajiri watu sahihi kwenye nafasi sahihi. Hata kwenye mpira hatusemi mchezaji fulani ni bora kwa sababu anacheza peke yake, bali ni muunganiko wa timu.

4. Mtu wa kwanza hupata yai wa pili hupata kiota.
Kama umewahi kuhudhuria au kushiriki mashindano yoyote utakuwa walau unajua hili. Mtu wa kwanza huwa anapata zawadi kubwa sana ambayo huwezi kuilinganisha na mtu wa pili. Vivyo hivyo kwenye biashara, mtu wa kwanza kufika eneo husika ndiye anapata shavu kubwa kuliko wale wanaofuatia baada yake.

Sasa utawezaje kuwa wa kwanza kufika eneo husika. Jiambie kauli ambayo mwanafalsafa mmmoja alikuwa akijiambia “ninataka nijue dunia inaenda wapi ili niwe wa kwanza kufika huko kabla ya mwingine”.

5. Usisubiri kukubaliwa na kila mtu. Nafsi yako ikikubali kitu basi kiendee.

Ukisubiri watu wakukubalie kufanya kitu fulani basi jua kwamba utasubiri sana. Wapo watu wanaokuonea huruma na hivyo hawataki uchukue hatua. Hivyo cha kufanya ukijiridhisha kwamba unaweza kuchukua hatua fulani na jambo hilo halivunji sheria ya nchi, basi kakifanye. Ni bora kuomba msamaha kuliko ruhusa.

6. Pale unapoweka nguvu na akili yako panakua. Hivyo kuwa makini kwenye vitu unavyoamua kufikiria, kufanya, kusikiliza, kuangalia n.k

7. Hakuna mwanadamu ambaye huwa anakuwa tajiri bila kuwasaidia wengine.

Tena kuthibitisha hili Zig Ziglar alisema hivi,  “unaweza kupata chochote ambacho Unataka kama upo tayari kuwaidia wengi kupata kile ambacho wanakitaka.

8. Kadri siku zinavyoenda  unapaswa kuachana na kusikiliza maneno ya watu. Jiskilize mwenyewe.

9. Kama unatafuta maisha yenye furaha basi weka malengo makubwa na yanayokuvutia.

Huu ndio ushauri kutoka mwanaviwanda wetu was siku zote Andre Carnegie. Ni huu yako kuutumia

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X