Kati ya vifaa vizuri ambavyo tunavyo kwenye zama hizi hapa basi ni Simu za mkononi na kampyuta. Vifaa hivi ni muhimu sana maana vinarahisisha maisha lakini pia vinasogeza taarifa karibu.
Tatizo linakuja linawakuta watumiaji wa vyombo hivi kiasi kwamba wanakuwa mateja.
Kwa sasa sio jambo la kushangaza kukuta watu waliopanga na wametumia nauli zao kutoka mbali ila sasa kinachofanyika baada ya kukaa chini ni kila mtu kuingia mtandaoni au kuongea na simu. Sijui ndio ukisasa au vipi! Mtu mmoja amewahi kusema kwamba “simu zimewaunganisha watu walio mbali na kuwatenganisha wale was karibu” mwingine akakazia kwa kusema, “wanadamu tunatengeneza vifaa, mwisho was siku vinatutengeneza”.
Vyombo hivi vimewashikilia watu kiasi kwamba sio rahisi tena kwa watu hawa kufikiri tena. Badala yake muda mwingi wanautumia huku kwenye mitandao ya kijamii hata pale wanapokuwa na kazi za maana. Kwa hakika zama zimebadilika na watu wameshikiliwa haswa.
Miongoni mwa ishara za kushikiliwa na mitandao ni pale ambapo mtu anapokwambia siwezi kumaliza siku bila kuingia mtandaoni. Au pale unapoweka picha na kila mara unashawishika kuangalia watu waliopigia kura (likes and comments).
Au pale unapokuwa unajua kwamba kuweka akiba ni muhimu ila wewe unaamua kuachana na kuweka akiba badala yake unanunua kifurushi.
Sasa cha kushangaza ni kwamba watu wameacha kujifunza ila mashine zinajifunza kuliko watu. Ndio maana kwa Sasa ukiingia mtandaoni mfano you tube. Utashangaa unaletewa kitu fulani kinachoendana na vile ambavyo unapenda. Wewe utakachofanya ni kubonyeza huku ukifurahi kumbe mashine zipo zinajifunza kutoka kwako.
Uamuzi wowote unaochukua zenyewe zinatunza. Siku nyingine ukirudi zinakuletea kitu kama kile ambacho uliakuwa unaangalia zamani. Loooo! Jambo hili linawafanya watu wazidi kuwa wateja zaidi wa mitandao. Kila mtu akitaka kutoka mtandaoni basi anaoneshwa kitu kizuri zaidi. Kumbe mashine zimeahakusoma zinachofanya ni kukuletea unachotaka ili uendelee kuwepo mtandaoni.
Jambo hili linawafanya watu wapunguze usanifu kazini.
Wengine wanaahindwa kutimiza majukumu yao. Wengine wanaunguza vyakula. Na wengine wanasahau watoto wao. Kwa hakika zama zimebadilika.
Sasa hapa kuna mambo ambayo ningependa uyazingatie ili wewe mtu was kujifunza zaidi kuliko mashine
Soma Zaidi; Zama Zimebadilika, Unafanya Nini Ili Mabadiliko Haya Yasikuathiri
1. Tenga muda maalumu wa kuingia mtandaoni. Ukiisha ndio umeisha endelea na kazi zako.
2. Usiingie mtandaoni mpaka utakapokuwa umemaliza kazi. Mtandao uwe zawadi baada ya wewe kutimiza majukumu yako ya kila siku.
3. Tafuta kitabu kimoja na hakikisha unakisoma mwanzo mpaka mwisho.
4. Usiingie mtandaoni asubuhi asubuhi.
5. Soma kitabu cha jinsi ya kuibua ubunifu ulio ndani yako.
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA