Masomo Saba (07) Ya Kujifunza Kutoka Kwa Wajasiliamali Wakubwa


“Kila mtu atapaswa kufanya walau kitu kimoja kikubwa katika maisha yake” huu ulikuwa ni wosia wa  Sakichi Toyoda kwa wanae  Kiichiro Toyoda.

Sakichi alikuwa ameanzisha kampuni ndogo ya kutengeneza vifaa vya magari na sasa wakati miaka inaenda na anakaribia kifo chake basi ikabidi atoe wosia huu kwa mwanae. Wosia huu uliambatana na kumkabidhi mwanae biashara yake ndogo ya kutengeneza vifaa vya magari. Kitu kikubwa ambacho Saikichi alikuwa anataka kutoka kwa mwanae ni kwamba aikuze biashara ile kwa kuchukua hatua kubwa. Ndio maana saikiro alimalizia kwa kumwambia mwanae hivi , nimetumia muda mwingi katika kubuni na kuboresha vifaa hivi, nategemea na wewe utafanya makubwa.

Kiichiro Toyoda alikuwa anaonekana kama zezeta fulani hivi na mtu ambaye hana ujuzi wa uongozi na wala hakutegemewa kabisa kwamba angeweza kufanya makubwa.  Lakini historia leo inaonesha ndiye mwanzilishi wa kampuni kubwa la magari aina ya TOYOTA.

Kwa nini nimeandika kuhusu Toyota? Hii ina uhusiano gani na kile ambacho napenda tujifunze siku ya leo?
Kwanza kabisa kuna kitu ambacho napenda tujifunze kwa pamoja. Pili napenda tuchukue hatua baada ya hapa ili kupata matokeo makubwa.

1. Kabla ya kuanzisha biashara unapaswa kujua kwamba unaingia katika kitu usichokijua na hivyo uwe tayari kujifunza. Jambo hili nimejifunza kwa mtu mmoja anayeitwa Elon Musk ambaye ni mwanzilishi wa makampuni ya Tesla, SpaceX na solar city.

2. Kabla ya kuanzisha biashara unapaswa kuwafikiria wateja wako, utavyowafikia na jinsi utakavyogusa maisha yao. Jambo hili nimejifunza kutoka kwa Kiichiro Toyoda ambaye alikuwa tayari kubadilisha jina lake ili liweze kutamkika na kuandikwa vizuri na watu wote. Mwanzoni kampuni hii iliitwa Toyoda lakini kwa sababu alitaka kampuni hii ifike hata kwa watu wanaoongea kiingereza basi aliamua kuiita Toyota.

3. Kabla kuanzisha biashara unapaswa kujua kwamba utapaswa kujitoa haswa. Utapaswa kufanya liwezekanalo ili kuhakikisha jina la biashara yako linabaki juu. Isije ikatokea kwamba biashara yako imekufa afu ndio unakuja kukumbuka kwamba ungeweza kufanya kitu ila hujafanya. Jambo hili nimejifunza kutoka kwa Elon Musk.

4. Biashara ni matangazo. Utapaswa kujitahidi kutangaza sana kile ambacho unafanya ili uweze kuuza.
Thomas Edison alikuwa mtaalamu wa jambo hili ukilinganisha na wagunduzi wengine wa nyakati zake kama Tesla. Edison alifanikiwa sana kutokana na ugunduzi wake. Kitu kilichochewa na uthubutu wake wa kutangaza biashara zake.

 5.  Wewe na biashara ni watu wawili tofauti. Kinachokuunganisha wewe na biashara ni kwamba wewe ni mwanzilishi na mwendeshaji. Usitoe hela ya biashara na kuitumia hovyo.

6. Asilimia 80 ya pesa inayotoka kwenye biashara yako itapaswa kurudi walau kwa mwaka mmoja wa kwanza. Hii ni kwa ajili ya kuipanua biashara yako na kuifanya isogee mbali zaidi. Ukitaka kujifunza hili kwa undani basi kutana na mtu anayeitwa Strive Masiyiwa, bilionea mwanzilishi wa Econet Wireless

7. Usianzishe biashara nyingi kwa wakati mmoja. Anzisha biashara kwa wakati ikisimama nenda kwa biashara ifuatayo. Richard Branson ni mfano mzuri huu ya hili. Ameweza kuanzisha makampuni makubwa na mengi ila kila kampuni limeanzishwa baada ya kuwa amesimamisha la awali.

Soma Zaidi; Watanzania Acheni Utani Tamthilia Hazijengi

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X