Tumia Vyema Rasilimali Zilizopo


Ukitaka kufanya mambo makubwa basi kuwa tayari kabisa kutumia raslimali ulizonazo. Kuna vitu vingi ambavyo kwa Sasa vimekuzunguka na unaweza kuanza kuvitumia hivi kuweza kufikia mafanikio makubwa maishani mwako. Labda unaweza kujiuliza hivi mimi nina raslimali gani?

Lakini pia mimi nikuulize wewe unataka kufanya nini? Anza kwa kujua ni kitu gani unataka kufanya maishani. Ukishajua kitu ambacho unataka kufanya sasa kifuatacho ni wewe kuangalia rasilimali zilizopo ili uanze kwa kuzitumia hizi.

Nilikuwa nasoma historia (biography) ya Thomas Edison ambaye ni mgunduzi wa vitu vingi sana ikiwemo taa ya umeme. Japo nimejifunza mengi  kutoka kwa Thomas Edison, ila moja ya kitu cha muhimu sana ni matumizi ya rasilimali zilizotuzunguka. Thomas alianza kuitumia nyumba yao kama maabara. Baadae aliitumia treni kama maabara. Baadae alikuwa anatumia ofisi  ya ajira yake kwa ajili ya kufanya utafiti na uchunguzi. Japo kila sehemu ilikuwa na changamoto zake, ila Thomas Edison hakuwahi kuacha kuangalia mazingira yake kama sehemu yake yeye kuanzia biashara hata siku moja. Alijisukuma zaidi na zaidi ili kufanya makubwa kwa kutumia rasilimali zilizopo. Je, wewe unazijua raslimali zilizokuzunguka? Unazitumiaje?

Soma zaidi; Muda Mzuri Wa Kuanza Jambo Lolote

Juu ya hili Zig Ziglar anasema, “anza kwa na kile ulichonacho, fanya kinachowezekana mwisho wa siku utajikuta unafanya yasiyowekekana”. Inawezekana ila anza sasa hivi

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X