Ukiweza Kumpa Mtu Kitu Hiki , Basi Utapata Chochote Unachotaka Kutoka Kwake


Kila mtu huwa kuna kitu ambacho anapendelea zaidi ya mwingine. Unaweza kukuta huyu anapenda mziki, lakini mwingine akawa anapenda kusafiri.
Moja ya kitu ambacho utapaswa kujifunza katika maisha basi ni kuwapa watu  kitu ambacho wanataka.

Hili sio tu kwa watu. Hata mvuvi anajua ili kumpata samaki basi atapaswa kumpa chambo. Sio kwa sababu eti anapenda maziwa basi samaki ampe maziwa. Samaki anakamata kwa kumpa chambo.  Vivyo hivyo kwa watu, ukitaka kuvutia watu zaidi kwako basi wape wanachopenda.

Sasa swali watu wanapenda nini?
Watu wanapenda kuonekana ni wa muhimu. Kitu hiki ndicho kinawasukuma watu kuvaa vizuri, kitu hiki kinawasukuma watu kusoma mpaka kupata vyeo vikubwa. Kitu hiki pia ndicho kinasukuma watu kutafuta hela.

Kwa hiyo kazi yako iwe ni kuwaonesha watu kwamba wao ni muhimu sana. Waoneshe watu kwa vitendo haswa juu ya umuhimu wao.
Wasifie kwa jinsi walivyo, kwa uvaaji wao. Onesha kuonesha kupenda jambo fulani ambalo wamelifanya siku za hivi karibuni.
Kumbuka tarehe zao za kuzaliwa, za watoto wao na wachumba wao.

Waandikie barua ya kuwapongeza juu ya jambo fulani au tukio la hivi karibuni. Nikuhakikishie ukifanya hivi utakuwa umefanya jambo la kipekee kwenye mahusiano ya binadamu na wewe utavuta watu wengi kwako.

Soma Zaidi: Mwandikie Mtu Huyu Barua Ya Kurasa Mbili Leo

Anza kufanyia kazi hili ambalo nimekushikisha siku hii ya leo.

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X