Badili Fikra zako Ili Ubadili Maisha Yako


Mwandishi nguli wa vitabu anayejulikana kama Napoleon Hill, alikiita kitabu chake THINK AND GROW RICH. Ikiwa na maana kwamba fikiri na uwe tajiri. Najiuliza “hivi kwa nini mwandishi huyu hakuiita kitabu hiki, FANYA KAZI KWA BIDII ILI UWE TAJIRI.
au kwa nini hakukiita, jitume sana ili uwe tajiri.
Au pengine kukiita pambana uwe tajiri.

Alitumia tu neno fikiri. Neno ambalo linahitaji ubadili fikra zetu ili kwenda hatua ya ziada. Au kiufupi neno ambao linatutaka tubadilike kwa ndani kwanza kabla ya kubadilika kwa nje.

 Kumbe kinachombadilisha mtu au kinachofanya mtu tajiri sio kufanya kazi kwa bidii, kujituma na kupambana.

Kitu nambari moja kitakachofanya maisha yako yawe ya kipekee sana ni wewe kubadili fikra zako (kubadili mwonekano wa ndani kabla ya mwoneoano wa nje). Mwandishi Brian Tracy, alikazia juu ya hili alipoandika kitabu chake na kukipa kichwa cha Badili fikra zako ili ubadili maisha yako.

Ni kutokana na kubadili fikra unaweza kujikuta unapaswa kuweka juhudi zaidi sehemu fulani ili uweze kusonga mbele zaidi.

Fikra ndizo huwatifautisha masikini na matajiri.
Watu wawili wanaweza kuingia kwenye mji mmoja na kukuta kwamba usafiri ni shida.

Mmoja akasema, “huu mji haufai kabisa, yaani usafiri wa shida na unasumbua kweli kutoka eneo moja kwenda jingine”

Ila mwingine akasema, “watu wa mji huu hawana usafiri, hii ni fursa kwangu kuwaletea usafiri ili niwarahisishie maisha. Watanilipa kwa kupanda usafiri na mimi nitakuwa tajiri”

Unaweza kuona kutokana na mifano huo hapo, mmoja ana fikra chanya, wakati mwingine anaona tatizo na anaendela kulalamika.

Siku zote ukikutana na tatizo, basi kuwa tayari kulibadili maana siku zote matatizo si tatizo bali ni daraja.

Chagua  kubadili fikra kwanza, ili ubadili maisha yako

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X