Chagua Kutoumizwa Na Kitu chochote


Choose not to be harmed and you won’t be harmed.
Don’t feel harmed and you haven’t been harmed

MARCUS AURELIUS

Katika maisha huwa nyakati ambazo huwa zinaambatana na changamoto kubwa sana. Ni katika nyakati hizi watu wengi huwa wanakata tamaa ya maisha, kupoteza mwelekeo na kujihusisha na vitu vibaya.

Ila ukweli nyakati kama hizi zipo kutuimarisha. Kikubwa tunapaswa kuwa wasikivu na kutafuta kujua ujumbe unaotokana na kikwazo ambacho kimetokea kwa wakati husika.
Kuna watu wengi sana wamekuja kuwa wabunifu wakubwa baada ya kuwa wamepitia nyakati ngumu.

Ukweli ni kwamba nyakati ngumu huwa haziishi. Ila ujumbe tunaopata baada ya kuwa tumepitia nyakati hizi unadumu milele.
Kwa hiyo ukikutana na nyakati ngumu, basi chagua kutoumia. Jua kwamba ni hali ambayo unapaswa kuipitia kwa wakati husika ili uwe bora zaidi.

Chuma hupitia kwenye moto mkali, (ambao tunaweza kusema ni wakati mgumu).
Ila kikitoka kinakuwa imara zaidi kuliko awali.

Kwa hiyo na wewe ukikutana na changamoto kwenye maisha chagua kutoumia maana hiyo ni sehemu ya kukuimarisha wewe zaidi.

Asante sana,

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X