Hatua Muhimu Za Kuchukua Unapojikuta Una Mambo Mengi Ya Kufanya Na Muda Ni Mchache


Mambo ni mengi, muda ni mchache. Huu ni usemi ambao unapata umaarufu sasa hivi. Labda swali ambalo tunapaswa kujiuliza sasa hivi, Je, mambo ndio yameanza kuwa mengi sasa hivi?

Mambo ni mengi siku zote. Hakuna siku ambapo mambo yamegeuka kuwa machache. Watu pekee wenye mambo machache ni wale ambao wameaga dunia.

Kutokana na wingi huu wa mambo hupaswi kukaa chini ya kuishia tu kusema mambo ni mengi. Unapaswa kwanza kufahamu kwamba japo mambo ni mengi lakini sio yote yanayohitaji muda wako. Kwa hiyo ni mambo kidogo sana ambayo yanahitaji muda wako. Ukifanya hivi kwenye orodha ya yale mambo mengi sana utakuwa umeipunguza mwa kiasi kikubwa sana.
Kwa hiyo hatua ya kwanza ambayo unapaswa kuchukua ni kuorodhesha idadi ya shughuli zako zote ambazo zinahitaji muda wako. Baada yako punguza shughuli hizo mpaka zibaki walau tano, ambazo unajua kabisa zinakuhitaji wewe.

Pili, baada ya hapo kati ya yale machache angalia ni yapi ambayo ni LAZIMA ufanye wewe. Yaani yale ambayo usipofanya wewe hayatafanyika.

Pia angalia ni yapi ambayo unaweza kuyaelekeza kwako wengine. Kwa kufanya hivi utakuwa umepunguza majukumu mengi  uliyokuwa nayo na kubakiza machache.

Mwisho kwenye yale majukumu machache ambayo umebakiza, angalia ni jukumu gani utaanza kulifanya na lipi litafuata. Kwa kufanya hivi utakuwa umepangilia ratiba yako vizuri kabisa.

Soma Zaidi; Huku Ndipo Unapaswa Kuwekeza Asilimia Kubwa Ya Muda Wako

Rafiki yangu kubali mambo yawe mengi, ila usikubali kupoteza mwelekeo wako wa kufanya mambo ya msingi.

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X