Hii Ndio Hali Ambayo Huwa Naipata Nikiwa Naandika Makala Za Blogu Au Magazetini


Moja kati ya muda ambapo huwa ninakaa na kufikiria sana ni pale ninapoanza kuandika.

Kinachonifanya nifikiria sana ni pale ambapo huwa nafikiria makala hii itasomwa na
Raisi wa nchi lakini pia itasomwa na mtu wa kawaida kijijni.
Makala itasomwa na wasomi wa vyuo vikuu (wenye Phd) pamoja na watu walioishia darasa la kwanza au ambao hawajasoma darasa la kwanza kabisa.

Pia huwa nikifiria kwamba makala itasomwa na watanzania pamoja na watu wa nje ya nchi.
Sasa mkusanyiko huu huwa unanifanya nifikiri kwa kina sana. Huwa najua kabisa ninapaswa kuandika kitu ambacho kila atayekisoma asitoke bure. Yaani apate kitu ambacho kitabadili maisha yake. Sasa hapo lazima nifikirie hasa.
Hata ninapotaka kuandika kibwagizo fulani, lazima nione ni kwa jinsi gani kitawagusa wote hawa.

Hivyo mwisho wa uandishi huwa nahisi kama vile nimetua mzigo mzito sana. Wakati huo huo kwa ndani huwa nina hamasa kubwa sana na uso wenye tabasamu. Huwa ninaamini kwamba nikiandika kitu kinachonihamasisha mimi, basi lazima kitamhasisha na mwingine.

Nimeona nikushirikishe hili maana kila mtu huwa ana maoni tofauti kuhusu uandishi. Uandishi ni kazi ambayo inahitaji muda kujitoa na nidhamu kubwa. Ila usione haya ukadhani mambo magumu😀😀.

Mambo ni mazuri sana kwenye uandishi? Je, unapenda kuandika?
Niandikie kupitia songambele.smb@gmail.com

Karibu sana

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X