Hii Ndio Idadi Kamili ya Vitabu Unavyopaswa Kuwa Umesoma Kuhusu Pesa Tu


Moja kati ya somo ambalo wengi huwa hawapendi kuliongelea sana ni pesa. Hata wale ambao huwa wanaiongelea basi huwa wanaiongelea kwa namna ambayo si sahihi.

Leo hii katika suala zima la pesa napenda ujue idadi ya vitabu unavyopaswa kuwa umesoma mpaka Sasa hivi. Maana kiwango cha pesa ulichonacho kinaendana na maarifa uliyonayo. Huwezi kupata pesa zaidi ya kiwango cha maarifa yako.

Na kwa kuwa maarifa yanapatikana kwenye vitabu basi leo hii napenda nikwambie idadi kamili ya vitabu unavyopaswa kuwa umesoma mpaka sasa hivi.

Idadi ya vitabu hukusu pesa tu. Ninasema kuhusu pesa tu. Unavyopaswa kuwa umesoma mpaka sasa hivi inapaswa kuendana na umri wako. Yaani idadi ya vitabu vya pesa inapaswa kuwa ni (MIAKA YAKO MARA KUMI NA MBILI)
Kama una miaka 20 basi idadi ya vitabu vyako inapaswa kuwa (20 mara 12) sawa na vitabu 240.

Kwa lugha rahisi ni sawa na kusema, unapaswa kusoma kitabu kimoja tu kwa mwezi kuhusu pesa. Idadi hii haihusishi vitabu vya malengo, vipaji, uongozi na vitabu vinginevyo. Hii ni idadi ya vitabu vya pesa tu.

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X