Hivi Ndivyo Huwa Napata Mawazo Kuandika Ya Makala Kila Siku


Moja kati ya swali ambalo ninakutana nalo kila siku, ni swali la  “Je, ninapata wapi vitu vya kuandika kila siku”?

Huwa napenda kujibu swali kirahisi sana kama swali lenyewe lilivyo rahisi? Huwa nauliza watu unapata wapi cha kuongea kila siku?

Wengine huwa wanasema, unajua kuongea sio sawa na kuandika. Sasa hapa nataka kukuonesha wapi huwa napata mawazo ya kuandika. Utashangaa sana.
Kumbuka haya ni baadhi tu ya maeneo sio yote

1. Maongezi yangu na watu wengine. Hapa huwa napata mambo mengi sana ya kuandika. Huwa natumia kanuni kwamba unaweza kujifunza kitu kutoka kwa kila mtu. Hivyo nikikutana na mtu siwezi kukosa kitu cha kujifunza kutoka kwake, kitakachopelekea Mimi kuandika. Hata kama tutakutana kwa sekunde mbili.

 Wanasema  unapokuwa nyundo kila kitu hugeuka kuwa msumari, Sasa hicho ndio nafanya. Kwangu kila ninachokiona najiuliza ni nini naweza kuandika kutoka hapa?

2. Nasikiliza zaidi ya kuongea. Kuna kanuni inaitwa kanuni ya 60-40. Kanuni hii inasema hivi “tumia asilimia 60 kusikiliza na asilimia 40 kuongea”. Kwa kufanya utajifunza mengi sana na utapata mengi sana ya kuandika. Njia hii naitumia na wewe unaweza kuitumia

Sasa labda unajiuliza nisikilize nini?
Anza kuwasikiliza watu waliokuzunguka. Watu wanapenda kusikilizwa sana. Unapoongea na watu jitahidi kuweka simu pembeni ili upate kusikikiza zaidi.

Sikiliza sauti za vifaa mbalimbali kama pikipiki zinazopita, magari, ndege n.k

3. Nasoma vitabu. Hapa ndipo pazuri sana. Na nimekuwa nikiandika sana huu ya kusoma Vitabu. Kifupi ni kwamba unapaswa kuwa na kiu na kusoma kila siku.

4. Napenda kutembelea mazingira ya asili. Yaani huku ndipo penyewe sasa. Asili huwa haidanganyi utapata kujifunza mengi sana. Asili inahusisha vitu kama misitu, milima n.k kile ninachojifunza huku ndio nakuja kuandika

5. Napenda kujifunza kwa waliopiga hatua na ambao hawajapiga hatua.
Kwa aliyepiga hatua najifunza kitu gani napaswa kufanya kwenda ninapotaka kwenda.

Kwa ambaye hajafanikiwa najifunza nini cha kuepuka.

Kwa jinsi hii sitakuja kukosa cha kuandika hata siku moja.

Karibu sana

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X