Hivi Nidvyo Kazi Za Sanaa Zinavyoweza Kukufanya Ufanye Makubwa Sana


Binafsi ni mpenzi mzuri sana wa kazi za sanaa. Kazi hizi huwa zinanifanya nifikiri kwa kina sana na pengine huwa zinaniletea mawazo mengine ambayo ni bora zaidi kuliko yale niliyokuwa nayo awali.

Kuzitafakari kazi hizi hunifanya niweze kutuliza akili yangu sehemu moja na kujiona bora zaidi.
Wapo watu ambao hawaipendi sanaa kwa kusema wao ni wanasayansi, ila kwa maoni yangu. Sanaa ikiunganishwa na sayansi pamoja na teknolojia unapata kitu kimoja kizuri sana. Kwa hiyo sanaa na sayansi sio vitu ambavyo vimetengana kama tunavyofikiri ila akili zetu ndizo zimemua kuvifanya hivyo.

Ndio maana ukienda vyuoni masomo mengi ambayo unakuta ni yanahusisha sanaa na sayansi kwa wakati mmoja huwa yanafurahisha na yanapendwa sana. Hayachoshi. Na kama somo linahusisha sanaa na sayansi ila ukaamua kushughulika na upande mmoja tu, mfano sayansi peke yake na kukiacha kipengele cha sanaa halileti mvuto.

Sasa leo nimeikumbuka kazi moja ya sanaa ambayo nimeisoma miaka ya nyuma kidogo. Kazi hii ni shairi linalojulikana kama Hollow Heads,
Kipindi nasoma  kidato cha tatu na nne. Nilitokea kupenda mashairi kuliko mtu mwingine aliyekuwa amenizunguka. Nikawa nakariri mashairi yote bila kuacha hata nukta (ya kiswahili kwa kiingereza).
Kuna shairi moja lilinipa msemo ambao nilikuwa nautumia kila mara hata kama nilikutana na changamoto. Shairi hili ni la hollow heads. Na kwenye shairi hilo kulikuwa na neno linasema, “I WILL FIGHT UP TO THE LAST CELL”. Maana yake ni nitapambana mpaka sekunde ya mwisho.

Neno hilo lilinisukuma sana kufanya mambo mengi sana. Hata katikati ya changamoto yoyote nilijiambia, nitapambana mpaka dakika ya mwisho.

Leo hii na wewe unaweza kuutumia usemi huu kufanya makubwa. Kila mara jiambia nitapambana mpaka sekunde ya mwisho. Yaani ikitokea umeshindwa kwenye maisha isiwe kwa sababu kuna kitu ulikuwa unaweza kufanya ila hukufanya. Ila iwe ni baada ya wewe kufanya kila kitu. Na kushindwa kutokee kwamba njia zote ulizotumia basi zimeshindikana. Yaani usiwe wewe ambaye umeshindwa bali mbinu zenyewe ulizofanya ndizo zishindwe. Naomba nikwambie kitu rafiki, ukijituma kwa namna hii, yaani kwamba utapigana mpaka sekunde ya mwisho basi utajikuta ukiongeza juhudi sana kwa yale ambayo unafanya na kufanya kwa ubora zaidi.
Nikutakie siku njema sana. Pambana mpaka sekunde ya mwisho.

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X