Ni nani asiyependa matokeo makubwa? Ni nani? Kila mtu hupenda matokeo makubwa katika kila eneo la maisha.
Watu wanapenda mahusiano yenye mafanikio makubwa. Watu wanapenda elimu ya kiwango cha juu. Watu wanapenda kuwa hela kiasi ambacho hawataweza kupata hofu. Wanafunzi mashuleni wanapenda kupata ufaulu mkubwa na unaopendeza. Haya yote ni matokeo makubwa. Ila matokeo makubwa huwa hayaji tu kizembe kizembe. Matokeo makubwa ni hutokea pale penye juhudi, kujituma, nidhamu isiyotetereka, utunzaji mzuri wa muda na kufuata kanuni za kitu unachofanya. Ukifanya hivyo lazima tu, utapata matokeo makubwa.
Je, utapenda kupata matokeo makubwa? Fanya kwa kuzingatia ushauri huyo hapo huu. Asante sana,
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391