Leo hii akirudi mtu mmoja ambaye aliishi miaka 2,000 iloyopita na kuona kinachoendelea hapa duniani atashangaa sana.
Kila kitu kwake utakuwa mshangao. Sio tu namna tunavyovaa nguo nzuri bali pia tunavyolala mahali pazuri.
Sio tu namna tunavyowasiliana tukionana kwa simu bali pia usafiri wa mabasi, ndege na majini ulivyobadilika.
Yaani kila kitu kimebadilika kabisa. Hadi vyakula tunavyokula, hadi uzalishaji wa vyakula wenyewe. Kwa hakika zama zimebadilika sana.
Kuna kitu kimoja kinasukuma mabadiliko haya yote kutokea. Kitu hiki sio kingine bali shauku ya binadamu kutaka kuboresha zaidi kile walichonacho sasa hivi.
Watu wana shauku ya kutaka kufanya mabadiliko. Watu wana shauku ya kufanya majaribio.
Shauku hii ndio imeleta mabadiliko makubwa sana.
Shauku hii ndio ilimfanya mtu agundue moto.
Shauku hii ndio imeleta umeme.
Shauku hii ndio imeboresha kila nyanja ya maisha.
Sasa na wewe unapaswa kuwa na shauku ya namna hii. Kila siku tafuta namna ya kuboresha zaidi kile ambacho unafanya ili kiweze kuwa bora zaidi. Kama kila siku utafanya mabadiliko kidogo kidogo, kwa mwaka utakuwa umefanya mabadiliko makubwa sana. Na kwa kitu unachofanya kitakuwa kimekuwa bora zaidi. Kumbuka mabadiliko huwa hayatokei ndani ya siku moja tu kwa mwaka. Mabadliko ni endelevu, kila siku kila saa na kila sekunde.
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
One response to “Kitu Hiki Ndicho Kimefanya Maisha Kuzidi Kuboreshwa Kila Siku”
Ahsante sana kwa elimi,hakika hii ni blog bora zaidi natakiwa kuumbatana nayo.