Makala Maalum Kwa Watu Wenye Mpango Wa Kuomba Kazi Au Wanaoomba Kazi Sasa Hivi


Moja ya mbinu ambayo imezoeleka kwenye kuomba ni kuandika CV na kuituma kwa mwajiri mtarajiwa huku ukisubiri majibu. Kadri siku zinavyozidi kusogea njia hii inazidi kuwa ya kizamani kidogo na hivyo lazima kuwe na njia bora kabisa ya kuomba kazi tofauti na wengi walivyozoea lakini yenye uhakika.

Njia hii mpya ni kuomba kukutana na mwajiri wako mtarajiwa ana kwa ana. Unaweza kuomba kukutana naye kwa ajili ya mlo wa jioni au unaweza kumfuatilia kwa umakini na kujua huwa anapendelea kula wapi chakula cha jioni.  unaweza pia kufuatilia maeneo ambapo huwa anapenda kutumia wikendi yake.
Ukishajua hilo unaenda eneo hilo na kuhakikisha unakutana naye.
Hapa unaweza kuongea naye mambo mengi ila mwisho wa siku ukaanza kuonesha ujuzi wako kwako.

Hakikisha unaeleza nini unaweza kufanya kwa ubora zaidi ya wengine.
Kama kuna video ya  yako ukifanya jambo la kipekee ioneshe.
Njia hii inakuongezea uwezekano wa kupata kazi mara 10 mpaka 100 zaidi ya yule ambaye anayetuma CV na kutulia.
Je, una mpango wa kuomba kazi?
Hakikisha unafanya kama nilivyoelekeza hapo.
Karibu sana

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X