Kwenye kitabu chake cha think big, Ben Carson anaelezea kisa kilichomkuta siku moja.
Ipo hivi kuna jamaa alimfuata Ben Carson na kumwambia, “yaani wewe Ben, ukijua kitu hutulii. Unataka kila mtu ajue kwamba unajua”.
Sikumbuki vizuri Carson alimjibu nini huyu jamaa, ila leo napenda kusema kwamba kama kuna kitu unajua na unajificha hutaki kukionesha ni kosa.
Najaribu kufikiria kama Thomas Edison angejua utengezaji wa taa, kisha akakaa kimya. Sijui sijui sasa hali ungekuwaje?
Au kama Elon Musk wazo lake la kuwa na benki ya mtandaoni (PayPal) asingelifanyia kazi, nani angetengeza benki za mtandaoni?
Kwa hiyo jitahidi kufanyia kazi na kuonesha kile unachojua. Usiogope kwamba sio sahihi. Kama kitu sio sahihi kitaboreshwa mbele ya safari.
Tukutane kwenye jukwaa la wanafanikio
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
Godius Rweyongeza
0755848391