Tafakari ya Kufikirisha Kutoka Kwa Waziri Mkuu Wa Ufaransa


“Tone la wino linaweza kufanya mamilioni ya watu kufikiri”, alisema Gordon Bryon Noel (1788-1824) ambaye alikuwa mtunga mashairi wa uingereza. Na matone haya ya wino ambayo yanafikirisha yamejaa sana kwenye vitabu. Matokeo yake ni kwamba matone haya huweza kumfanya mtu kufikiri kwa kuweka mipango mikubwa, au matone haya pia huweza kumfanya mtu achukue hatua kubwa.

Kwa sasa nipo nasoma kitabu cha THE PARABLE OF DOLLARS. Kwenye kitabu hiki nimekutana na kauli ya kutafakarisha kutoka kwa waziri mkuu wa ufaransa. Kauli hii inasema hivi, “Tengeneza mipango mikubwa. Usiweke mipango midogo. Mipango mikubwa huvutia watu wakubwa. Mipango midogo huvutia watu wadogo na watu wadogo husababisha matatizo makubwa”.

Kutokana na kauli hii kuna mengi sana ya kujifunza.
1. Unapaswa kuwa na mipango mikubwa sana kwenye maisha yako.

2. Mipango mikubwa huvutia watu wakubwa. Wawekezaji wakubwa wanapenda kuwekeza kwenye mipango mikubwa. Kama wewe una mpango mdogo utavutia watu wadogo kama mpango wako ulivyo.

Lakini mwisho wa maneno haya yenye busara kutoka kwa waziri huyu mkuu kuna onyo. Tena hili ni onyo kali.
Anasema hivi, “mipango midogo huvutia watu wadogo NA WATU WADOGO HUSABABISHA MATATIZO MAKUBWA. Hili ni onyo kali.
Kama unataka matatizo kwenye maisha basi weka mipango midogo. Na matatizo utakayoyapata yatakuwa ni makubwa zaidi.
Ngoja nikuoneshe mfano wa mpango mdogo na madhara yake yalivyo makubwa

Chukulia umeishiwa hela . Sasa unaweka mpango mdogo wa kukopa. Unakopa ili ule. Baada ya hapo siku za kulipa deni zinafika ila bado hujawa na hela. Unaamua kukopa kwa mwingine ili kulipa deni. Wahenga wanasema unamuibia Petro kumlipa Paulo.
Kwa hiyo unajikuta mchezo unaendelea bila kikomo. Hayo ndiyo madhara ya mipango midogo. Ila kama ungekuwa na mipango mikubwa.
Ungejiuliza nini chanzo cha mimi kukosa hela! Je, nifanye nini ili kupata hela kuondoa huu uhaba nilionao.
Mwisho wa siku ungejikuta umekuja na wazo kubwa ambalo lingetatua tatizo mwanzo mwisho.

Kuanzia leo. Sema kwamba mipango midogo mwisho.
Karibu mipango mikubwa. Maisha yanajegwa kwenye nguzo za mipango mikubwa.

Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.
MIPANGO MIKUBWA + HATUA KUBWA=MATOKEO MAKUBWA kinyume chake
MIPANGO MIDOGO +HATUA NDOGO =MATATIZO MAKUBWA.

Soma Zaidi: TAFAKARI YA WIKI: Kipaji Ni Bei Rahisi Sana Kuliko Chumvi

Chagua kuwa na mipango mikubwa.

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X