Kuna misemo mingi sana ya wahenga na kila usemi huwa unakuta umebeba ujumbe fulani. Sasa leo hii tunakutana na usemi unaosema, “unamwibia Petro kumlipa Paulo”.
Katika maisha kuna vitu unafanya ambavyo kwa hakika ni vya kumwibia Petro ili Kumlipa Paulo.
Mfano umeishiwa na hela na unachokimbilia kufanya ni kukopa. Hapa unakuwa unakimbilia kuzima moto kwa haraka haraka (sawa na wizi). Ila madhara yake yanakuja kuwa makubwa kwako.
Au umekutana na changamoto. Usikimbilie kunywa pombe au kilevi ili uondokane na tatizo hilo. Hapo unakuwa unatengeneza tatizo zaidi. Huwezi kutatua tatizo kwa kuongeza tatizo, hiyo ni sawa na kumwibia Petro kumlipa Paulo.
Jiepushe sana kumwibia Petro kwenye maisha yako ili umlipe Paulo.
Siku zote inapotokea tatizo, tafuta chanzo chake. Litatue na songa mbele. Asante sana.
One response to “TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA tatizo unamwibia Petro Kumlipa Paulo”
[…] SOMA ZAIDI: TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA tatizo unamwibia Petro Kumlipa Paulo […]