Usiogope Kushindwa, Ni Sehemu Ya Kujifunza


Thomas Edison anafahamika kwa ubunifu wake wa vitu vingi sana. Moja kati ya kauli yake ambayo amewahi kuisema ni hii hapa, “siku zote naogopa vitu ambavyo huwa nagusa mara ya kwanza na vinafanya kazi pale pale”.

Maana yake, nini? Maana yake vitu hivyo havijakupa nafasi ya kujifunza. Na havijakupa nafasi ya kukua zaidi.

Sio kwamba ukifanya kitu mara moja kikafanikiwa inakuwa sio sahihi, hapana. Ila napenda ujue kwamba ikitokea umeshindwa usilie. Ni sehemu ya wewe kujua zaidi.
Ni katika hali za sintofahamu kama hizi hapa, watu huwa tunapata nafasi ya kukua zaidi.

Ukianguka, usikae chini. Dunda juu uendelee na safari.

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X