Huu Ndio Ukombozi Muhimu Ambao Wewe Hapo Unauhitaji


Neno ukombozi kwenye kamusi ya kiswahili sanifu linamaanisha, UOKOAJI WA WA WATU KUTOKA KWENYE HALI MBAYA AU DUNI.

Kumbe makala ya leo imejikita katika kuhakikisha unaelewa nini unapaswa kufanya ili kutoka kwenye hali mbaya.
Je, ni aina gani ya ukombozi unaihitaji?
Kitu  kikubwa ambacho kinahitajika ni wewe kukombolewa kifikra. Ndio fikra zako ni kitu cha kwanza kabisa ambacho wewe hapo unahitaji. Na ukombozi wa fikra hauji tu hivihivi. Ukombozi wa fikra unakuja kwa wewe kupata maarifa sahihi. Maarifa sahihi ndio yatakupelekea wewe kuchukua hatua sahihi.
Maarifa sahihi ndio yatakupelekea wewe kufanya maamuzi sahihi.

Huwa ninapenda kusema kwamba maarifa sahihi + hatua kubwa na sahihi huleta matokeo makubwa. Na huu ni ukweli.

Kwa hiyo kila siku tafuta kuhakikisha unapata maarifa sahihi. Ukishapata maarifa sahihi yafanyie kazi.

Labda utajiuliza ni wapi naweza kupata maarifa sahihi? Nipende kukwambia kwamba maarifa sahihi yanapatikana kwenye vitabu. Tafuta Vitabu sahihi usome. Soma soma na soma vitabu. Huku utapata maarifa sahihi ambayo yatakupa ukombozi wa fikra.

Asante sana. Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

Karibu sana
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X