Kitabu Muhimu Unachopaswa Kusoma Kuhusu Ubunifu


Ubunifu ni mbegu ambayo kila mtu anayo ndani yake. Mbegu hii inahitaji kuwekewa mazingira mazuri sana ili ikue na kutoa matunda.

Mbegu ya kawaida ambayo hupandwa shambani huhitaji maji, hewa, jotoridi na virutubisho ili kuota. Ila maji, hewa, jotoridi  na virutubisho vya ubunifu ulio ndani yako ni tofauti na hivi vinavyohitajika na mbegu za kawaida. Mbegu za ubunifu ulio ndani yako zinahitaji vitu zaidi ya thelathini. Nimevieleza vitu hivi kwa undani kwenye kitabu cha JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO. Kinapatikana kwa sh, 7,000/-. Tuwasiliane.

Ila leo kuna kitabu cha ziada ambacho ninaenda kukutumia bure kabisa. Kitabu hiki sio kingine Bali ni kitabu IBA KAMA MSANII (STEAL LIKE AN ARTIST).
Unaruhusiwa kuiba. Ila sasa iba kama msanii.

Kama wewe ni mfuatiliaji wa muziki utakuwa umewahi kusikia watu wanasema Diamond ameigizia wimbo fulani kutoka kwa msanii fulani.
Kitu hiki kwa lugha ya kisanii ndicho kinaitwa kuiba kisanii. Kinaruhusiwa.
Unajua wasanii wanaibaje?
Ngoja Sasa hapa nikwambie wanavyoiba
1. Wanasoma sana
2.wanawakubali wale waliowaibia
3. Wanaiba kutoka kwa wengi
4. Wanabuni kitu cha awali na kutengeneza kitu kingine kipya kabisa

Bila shaka unaifahamu treni. Treni imeibwa kutoka kwa jongoo, lakini ni wachache sana wanaweza kugundua hilo.

Huo ndio wizi wa kisanii na huo ndio wizi ambao unapaswa kuufanya.

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X