Usitafute Kiki Kwa Kutengeneza Matatizo


Kama unataka kufanya mambo makubwa na kujulikana basi usitengeneze matatizo ili upate nafasi ya kujulikana.
Namna nzuri na inayodumu na ambayo imetumiwa na watu wote wa mfano kwenye dunia hii ni kutatua matatizo.

Kwa hiyo wewe siku zote tafuta matatizo ambayo yanawakumba watu kwenye jamii. Tatua haya matatizo vizuri kabisa. Kumbuka kwamba matatizo ya jamii sio matatizo.
Matatizo ni biashara,
Matatizo ni fursa
Matatizo ni tuta katika barabara ambalo ukilivuka unaongeza mwendo.

Hivyo usiogope kutatua matatizo. Kuwa sehemu ya suluhisho. Kama kweli unapenda kutafuta kiki, basi tafuta kiki kwa kuisaidia jamii.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X