Hakuna Mafanikio Bila Kujitoa Sadaka


Hakuwezi kuwepo naafanikio makubwa bila ya mtu kujitoa sadaka nankuachana na vile vitu ambavyo anavipenda kwa muda ili aweze kupata mafanikio makubwa baadae.

Unapaswa kujitoa sadaka kwa kuachana na mawazo hasi na kuweka nguvu zako na muda wako kayika kufanya mambo ya maana. kama utawekabngugu zako na muda wako katika kufanya mambo ya maana, hamna jinsi lazima tu utaweza kufanikiwa. Mafanikio lazima yatakuja kama utaamua kuachana na vitu vidogo ambavyo havina maana.

Eric Shigongo James ameandika katika Kitabu chake kwamba, kuna watu kwa sababu ya tabia zao umasikini utaendelea kuwaandama tu na kuna watu kwa sababu tabia hata waukimbie utajiri utawafuata tu.

Unajua moja ya kitu kinachowafanya watu wafanikiwe na kuwa Matajiri ni kipi?
Ni kujitoa sadaka

1. Wanajitoa sadaka kwa kusoma Vitabu
2. Wanajitoa sadaka ya kuweka akiba
3. Wanajitoa sadaka ya kuachana na taarifa za habari na magazeti
4. Wanajitoa sadaka kwa kuachana na mahusiano ambayo sio mazuri
5. Wanajitoa sadaka kwa  kula Chakula bora
6. Wanajitoa sadaka kwa kuamka mapema
7. Wanajitoa sadaka kwa kuamua kufuatilia mambo yao na kuachana na mambo ya watu wengine.

Je, wewe upo tayari kujitoa sadaka kwa kufanya nini?

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X