Hii Ni Kauli Ya Kishujaa Ambayo Unaweza Kuisema Unapokuwa Umekwama Na Watu Wanaonekana Kwenda Kinyume Chako


Watu wenye ndoto kubwa sana huwa wanafika sehemu ambapo wanakwama kabisa na hali huwa inaonekana kwenda kunyume na matarajio yao. Hapo ndipo watu waliokuwa wakiwaamini tangu mwanzo huanza kuonesha mashaka na pengine kutaka kuwakimbia.  Kiukweli ni kipindi kigumu ambacho watu hawa hupitia ila kwa sababu wana ndoto kubwa wanavumilia na hatimaye kwenda wanapotaka.

Hiki ndicho kilimtokea Steve Jobs, mwanzoni mwa miaka ya tisini. Kampuni yake ya NEXT ilikuwa inaanguka vibaya sana na kila mtu alipoteza ile imani aliyokuwa nayo kwa Steve Jobs. Hata wale waanzilishi wa kampuni walimkimbia. Wafanyakazi wengine walikimbia na kuanza kuona kama mtu ambaye amepoteza mwelekeo na mtu ambaye hataweza kufanya makubwa tena maishani.
Hapo ndipo Steve Jobs alisimama wima na kuwaambia wafanyakazi wa wawekezaji na waanzilishi wengine wa kampuni. Alisema, “kila mtu anaweza kuondoka hapa isipokuwa mimi tu”.
Hii ni kauli ya kishujaa unapokuwa unaendea ndoto zako. Hii ni kauli ambayo itaonesha bado unaamini katika ndoto zako na unaweza kwenda mbali zaidi. Kauli hii itaongeza nguvu na kuwafanya hata wale waliokuwa wanataka kukukimbia basi wajihoji na kurudi nyuma kidogo.

Hali kama hiyo iliyomtokea Steve Jobs imewahi pia kutokea Jack Ma mwanzoni mwa miaka ya 2000. Kampumi yake ilikuwa inaonekana kama inakufa na haikuwa na mwelekeo mzuri. Jack Ma alisimama wima na kusema,
Ambaye anaona kampuni inakuga aondoke.
Ambaye amesubiri kampuni ipelekwe IPO ili apate pesa aondoke.
Ambaye anakuja hapa kufanya kazi bila kuwa na imani na kampuni aondoke.
Ambaye hapendi kazi anayoifanya aondoke.

Kwani unadhani kuna aliyeondoka? Watu wote ilibidi wakae maana shujaa wao alishaonesha anaamini kile anachofanya na atakipigania mpaka mwisho.
Kauli hizi zimetolewa na watu tofauti ila maana yake bado ni ile ile.

Kwa hiyo na wewe unaweza kuchagua mojawapo na kuitumia au ukatumia zote kwa wakati mmoja. Ni hivyo tu rafiki yangu.

Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

Asante.

 Kama bado hujajiunga na mfumo wetu wa kutokea Makala maalum kwa watu maalum BONYEZA HAPA
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X