Hili Ni Jina Ambalo Unapaswa Kuacha Kulazimisha Kujiita


Siku hizi kumekuwepo na watu wengi ambao wanajiita wajasiliamali. Uwepo wa mitandao ya kijamii pia umerahisisha hili kwa kufanya watu wengi waandike kwenye akaunti zao kwamba wao ni wajasiliamali. Pengine utakuta mtu anajitambulisha kwa watu kwamba yeye ni mjasiliamali. Yaani ujasiliamali umekuwa kama cheo vile. Kama vile watu wanavyoitwa daktari, mwalimu, waziri n.k Sasa pia inaelekea kuna cheo kipya cha mjasiliamali.

 Sasa labda tujiulize ni sahihi kujitambulisha kwa watu kwamba wewe ni mjasiliamali?
Kabla ya kujibu hili swali tujiulize, labda ujasiliamali ni nini? Ujasiliamali ni ile hali ya kutatua matatizo ya watu (hii ndio maana ya mjasiliamali kama ilivyo kwenye Kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI). Na ukiangalia wajasiliamali ambao wamewahi kugusa maisha ya watu hapa duniani hawakuwahi kujiita wajasiliamali. Fuatilia watu kama Thomas Edison, Henry Ford, Andrew Carnegie, Steve Jobs, John Rockefeller na wengineo wengi. Kamwe watu hawa hawakuwahi kujiita wajasiliamali Bali walichofanya ni kuuishi ujasiliamali, hivyo tu. Walitatua matatizo ya watu  na kusongambele.

Soma Zaidi: Vitu Vinne Vinavyowafanya Waajiriwa Kuendelea Kuajiriwa

Sasa ngoja turudi kwenye swali na tujiulize. Je, ni sahihi kujiita mjasiliamali. Jibu ni kwamba Sio sahihi. Weka nguvu kubwa sana katika kutenda zaidi kuliko kushawishi watu wakuone wewe kama mjasiliamali. Badala ya kutumia muda mwingi kushawishi watu kwamba wewe ni mjasiliamali, waoneshe watu kwamba wewe ni mjasiliamali.

Asante sana. Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X