Maisha ni mchezo ambao unapaswa kujua namna ya kuucheza. Hata hivyo mchezo huu una Sheria zake ambazo ni za kipekee sana. Hivyo unahitaji kuzifahamu Sheria hizi.
Kama ilivyo kwenye mchezo wa mpira wa miguu, sio kila mtu ni gwiji kwenye mchezo huyo. Vivyohivyo kwenye mchezo wa maisha. Sio kila mtu ni gwiji. Ila wewe unaweza kuugifikia ugwiji kwa kufanya yafuatayo.
1. Kusoma Vitabu na kujifunza kitu kipya kila siku.
Nimegundua watu wengi wanaofanya makubwa ni wasomaji wazuri wa vitabu. katika vitabu wanapata fikra mpya ambazo zinawafanya wasonge mbele. Ukikutana na Ben Carson, atakwambia soma Vitabu. Ukienda kwa Donald Trump atakwambia soma sana Vitabu. Ukikutana na Kamkwamba atasema, soma Vitabu kadri uwezavyo. Na Mimi ninasemaje? Soma Vitabu
2. Kuweka katika matendo yale uliyosoma kwenye vitabu.
Usiishie tu kuwa msomaji wa Vitabu, kuwa mtekelezaji wa kile unachosoalma. Kiweke katika matendo nankifanyie kazi zaidi ya mtu mwingine.
Haya ni mambo mawili ambayo kama utayafanyia kazi siku zote za maisha yako, basi utageuka kuwa gwiji