Huyu Ni Mtu Ambaye Unapaswa Kumfahamu Nje Ndani


Mara nyingi sana huwa tunajihusisha na vitu vingi sana. Unakuta mtu anafuatilia vitu vingi, kuanzia taarifa ya habari, kuangalia tamthiliya kufuatilia maisha ya watu mtandaoni na mambo mengine kadha wa kadha. Ila kuna mtu ambaye huwa unamsahau kumfuatilia kila siku. Na mtu huyu siye mwingine Bali wewe hapo. Yaani kabla hujafuatilia habari zilizotokea Darfur, au Kabla hujajua Trump kaongea nini. Unapaswa kuwa umejifahamu wewe kwanza.
Fahamu ni hatua gani umeweza kupiga. Ulikuwa wapi na wapi unataka kuelekea na ni vitu gani vinakukwamisha. Hivyo tu basi.

Kwa hiyo kuanzia leo, anza kujifanyia tathimini wewe mwenyewe ili ujue wapi upo na wapi unapaswa kwenda ili kuweza kufikia ndoto zako kubwa.

Asante sana rafiki tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X