Hivi umewahi kufanya jambo na kuona haiwezekani. Au umewahi kufanya jambo na kuishia njiani? Shida ilikuwa nini?
Inawezekana ulisema haiwezekani na ukaamua kuishia njiani. Ukweli ni kwamba hakuna kitu ambacho hakiwezekani ukiamua. Kila kitu kinawezekana.
Ila pale unaposema kwamba haiwezekani unakuwa unajiwekea kizuizi cha kusongambele na kufikia viwango vikubwa.
Sasa kinachotokea ni kwamba utakwama na kutulia. Wakati unaendelea na mkwamo wako utashangaa watu wasiojiwekea vikwazo akilini wanatimiza kile ulichosema hakiwezekani. Kwa hiyo nipende tu kusema kwamba hakuna kisichowezekana. Kila kitu kinawezekana kama utaamua. Kama bado hujajiunga na mfumo wetu wa kutokea Makala maalum kwa watu maalum BONYEZA HAPA