Kitu kibaya zaidi ya kutokuwa na macho ya kuona (utashangaa kusoma kitu hiki cha kipekee).


Hellen Keller (1880-1968)  alikuwa mwandishi, mwanasiasa na Mwalimu wa chuo. Kwa miaka hiyo alikuwa ni kipofu wa kwanza kupata shahada ya Chuo kikuu. Siku moja alitoa hotuba moja ambayo iligusa maisha ya watu. Baada ya hotuba hiyo waandishi walikusanyika ili kumuuliza maswali ya hapa na pale. Wakati maswali yanaendelea kuulizwa alijitoleza kijana mmoja ambaye alisafisha koo na kusogea mbele  kidogo. Kijana huyu alikuwa ameitafuta nafasi hii kwa muda mrefu  na isitoshe alikuwa mchanga kwenye ulimwengu wa habari. Aliuliza, “kitu gani ni kibaya zaidi katika maisha zaidi ya kuwa kipofu”.
Mara ghafla sauti ya miguno zikaanza kusikika. Mtu mmoja kwenye kundi la watu akasikika akisema, swali gani hilo achana nalo usilijibu. Mwingine akasema swali hilo linadhalilisha achana nalo.

Lakini hali haikuwa hivyo kwa Hellen Keller. Alionekana kulipenda swali na hivyo aliwaashiria watu watulie ili aweze kujibu hilo swali. Alisema, “kitu kibaya zaidi katika maisha ni kuwa na macho bila ya kuwa na maono/ndoto”.
Akamaliza.

Unajua nini? Kuna watu walifikiri  kitu kibaya zaidi ya kuona kitakuwa labda ulemavu wa mikono au miguu. Ila alisema maono au ndoto ndio kitu kibaya zaidi.

Swali kama hilo lingeulizwa kwa vijana wa zama  hizi  basi ungeshangaa. Kuna ambao wangesema kitu kibaya zaidi ni kutokuwa na mtaji wa kuanzisha biashafa, wengine wangesema kitu kibaya zaidi ya kukosa msaada wa serikali, wengine wangesema kitu kibaya zaidi ni kukosa elimu.

Tunachojifunza kwa Hellen Keller ni kwamba maono ni mwongozo wa maisha.  Mtu mmoja amewahi kusisitiza kwa kusema kuwa, maono au ndoto sio zile unazoota ukiwa umelala. Bali ni kile kitu ambacho unakiona na kukiendea hata kama umefumba macho. Tena wataalam wanasema ndoto zako zinapaswa kuwa kubwa zaidi kiasi cha kukuogopesa hata wewe. Ndoto kubwa ziyakufanya
1. Upate nguvu ya kusonga mbele hata pale mambo yanapokuwa ni magumu maishani mwako au unapokutana na changamoto

2. Zitakufanya upangilie muda wako kwa vipaumbele.

3. Zitakufanya utengeneze konekisheni za maana na kwa wakati.

4. Zitakufanya ubaki ukiwa na motisha ya kufanya makubwa kwa wakati wote.

Je, wewe ndoto zako kubwa ni zipi?

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X