Mambo 25 Niliyojifunza Ndani Ya Miaka 25 Ya Kuishi Kwangu Hapa Duniani


Mwaka 1994, tarehe 5/8 ilikuwa ni siku ambayo kwa mara ya kwanza nilizaliwa na kuvuta pumzi ya kwanza ya dunia hii. Na leo hii ndipo naadhimisha miaka 25 ya kuzaliwa kwangu. Niseme kwamba hii ni siku muhimu ambayo imenifanya niweze kuona mengi, kukutana na watu wengi na kuzunguka maeneneo mengi.

Miaka yangu ishirini na tano ya kwanza nimeitumia nikiwa shuleni. Kwa hiyo kitu kikubwa sana ambacho nimekifanya ndani ya miaka hii ni shule tu basi. Sasa.  Ndani ya miaka hii katika kusoma vitabu, kukutana na watu, kuongea na watu, kutembelea maeneo na kufanya vitu vingi sana nimepata kujifunza mambo ishirini na tano. Mambo haya ni muhimu sana kwangu, lakini pia wewe yataweza kukusaidia kufikia hatua kubwa.

1. Kila mtu amezaliwa na mbegu ya  ubunifu ambayo ipo ndani yake. Kama ilivyo kwa mbegu ya  kawaida inahitaji maji, hewa na jotoridi ili iweze kuota. Vivyo hivyo kwa mbegu ya ubunifu ambayo mimi na wewe tunayo, mbegu hii inahitaji kukuzwa kwa kuwekewa mazingira safi ambayo yataifanya iweze kuota kwa ubora zaidi, na mazingira haya ni kama kuipa muda wa kukua, kufanya mazoezi, na kujituma.

2. Muda mzuri sana wa wewe kuanza kufanya kitu  ni pale ambapo unapata wazo. Ukipata wazo liweke katika matendo na anza kulifanyia kazi mara moja. Huhitaji kusubiri kila kitu kiwe sawa.

3. Eneo lenye matatizo makubwa ni eneo ambalo lina fursa nyingi. Kitu kikubwa ambacho unahitaji ni kuhakikisha kwamba unatatua changamoto ambazo zinaikumba jamii yako.

4. Unapokuwa kijana, huku ukiwa na nguvu nyingi, unakuwa ndio muda mzuri kwako kujaribu  kufanya mambo mengi sana bila kuogopa. Jaribu vitu vingi kadri uwezavyo na vile vinavyofanya kazi endana navyo wakati vile ambavyo havifanyi kazi unaachana navyo.

5. Uoga ni kitu ambacho unakijenga wewe mwenyewe kwenye akili yako  ila kiukweli ni kwamba hakina uhalisia. Hivyo usioogope kitu au mtu yeyote. Watu ambao unawaogopa wewe, wanakuogopa na wewe pia.

6. Ukweli ni kwamba hata yule au watu wale ambao wewe unawaogoopa na wao wanakuogopa wewe.

7. Kila mtu ni kiongozi katika maisha bila kujali cheo chake. Uongozi  hauhitaji kuwa na cheo. Ila unahitaji wewe kupumua tu. Kuna vitu ambavyo unapaswa kuvifanyya hata kama hauna cheo na unapaswa kuvifanya kwa weredi mkubwa sana. Yawezekana wewe ni karani eneo fulani na hauna cheo ila ukiifanyakazi yako kwa ubora utakuwa umetimiza majukumu yako  kama kiongozi. Wewe kama kiongozi unahitaji kuhakikisha kwamba kila kitu ambacho unakigusa unakifanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Huhitaji cheo ili kutumia kipaji chako. Huhitaji cheo ili kutatua matatizo yanayoikumba jamii yako.

8. Haijalishi umeanzia wapi kwenye maisha, una uwezo wa kutengeneza kesho bora  kuanzia hapo ulipo na hatimaye kufikia hatua kubwa maishani. Kikubwa ambacho unapaswa kufahamu ni kwamba unapaswa kuanza na kile ulichonacho, kufanya kile ambacho kinawezekana ili hatimaye uweze kufanya kile ambacho wengine wanaona kwamba hakiwezekani kufanyika maishani.

  Kuna watu walikuwa ni  walinzi wa kampuni zao ila kwa kutumia hiyo fursa tu wamefikia hadi hatua ya kununua kampuni ambazo walikuwa wanafanya ulinzi hapo,

10. Fursa zipo kila mahali unapoenda. Na fursa zinakija kila wakati. Usifanye vitu kwa kukimbiakimbia bila mpango.  Na fursa fulani ikikupita usihuzunike. Kumbuka kwamba fursa ni kama daladala, likikupita moja litakuja jingine ambalo utapanda.

11. Usiipe nafasi chuki kwenye maisha yako.  Kama mtu atakukosea msamehe,usikae na chuki unajiukiza mwenyewe.

12. Ukimkumbuka mtu mjulie hali, ukimpenda mtu mwambie, mtu akikukosea msamehe maisha ni mafupi sana kwako kupoteza kwa mambo yasiyo na maana

13. Ni bora kuomba msamaha kuliko kuomba ruhusa. Mara nyingi unapokuwa unaanza kufanya kitu ambacho unacho kwenye ndoto zako kubwa, kuna watu watakuona kama umekengeka. Wapo watakaokukataza usifany kile ambacho unakifanya na wapo pia ambao watakucheka. Usiwasikiilize watu wa namna hii. Wewe fanya kitu ambacho unajua kabisa kwamba ni sahihi na hakivunji sheria za nchi. Kikifanikiwa kila mtu atafurahi sana ila kikikataa utaomba msamaha na kuendelea na kitu kingine. Kwa hiyo fahamu kwamba ni bora kuomba mshamaha kuliko kuomba ruhusa

14. Hakuna mtu anayeona unapoona wewe. Iwe ni mzazi, ndugu au jamaa. Kama wewe una ndoto kubwa sana usiwasilikilize watu. Kazana kutimiza ndoto zako.

15. Kuna vitu viwili  muhimu sana ambavyo unapaswa kuvifanya maishani wako. Moja ni kupanda miti pili ni kuandika Kitabu. Kama  utakosa kufanya vitu vingine vyote, basi fanya hivi.

16. Unapokuwa unafanya kazi au unatimiza majukumu fulani na ukaanza kujisikia kuchoka, ukweli ni kwamba unakuwa hujachokka bali hapo ndipo unapaswa kuanza kuhesabu moja na kuanza upya. Imethibitishwa kwamba unapojisikia kuchoka unakuwa umetumia asilimia 40 tu ya uwezo wako na unapaswa kujisukuma zaidi ili uweze kutumia asilimia 10 au 20 zaidi ili uweze kufanya mambo makubwa

17. Vitabu vina suluhisho la kila kitu ambacho wewe unakifahamu. Na watu wakubwa wote ambao unawafahamu walikuwa ni watu wa kusoma vitabu siku zote.  Ukiona mtu amefanikiwa jiulize anaasoma vitabu gani ambavyo mimi hapa sisomi. Ukisoma vitabu vya watu waliofanikiwa na wewe lazima utafanikiwa tu.

18. Sikiliza zaidi unavyoongea. Umeumbwa na masikio mawili na mdomo mmoja. Unapaswa kuwa mtu wa kusikiliza zaidi kuliko unavyoongea.  Na katika suala hili utahitaji kutumia kanuni ya 60-40. Ambapo kanuni hii inasema kwamba unapaswa kuwa msikilizaji zaidi ya unavyokuwa muongeaji. Yaani unapaswa kutumia asilimia 60 ya muda wako kusikiliza na asilimia 40 tu katika kuongea

19. Inawezekana kuishi bila kuangalia runinga wala kusikiliza redio. Na jambo hili nimeweza kulifanyia kazi na kuliishi kwa miaka mitatu iliyopita. Sijawahi kusikiliza runinga wala sina muda wa kusikiliza redio. Cha kushangaza ni kwamba sijawahi kukosa kitu chochote cha maana.

20. Usisubiri connection ili uanze. Tengeneza connection wewe mwenyewe.

21. Usilalamike. Usimlalamikie mzazi serikali au taasisi yotote. Kama kuna kitu hakifanyiki vizuri, tatizo ni wewe. Kama kuna kitu kinafanyika kwa ubora zaidi ni wewe umesababisha pia. Kumbuka, ukishinda ni juu yako. Ukishindwa pia ni juu yako.

22. Mtandao wa watu waliokuzunguka unaweza kukusukuma kufikia mafanikio au kushindwa kabisa. Kwa hiyo unapaswa kuwa makini sana unapochagua aina ya marafiki unaopaswa kuwa nao na kukuzunguka. Wanasema hivi, niambie rafiki yako nikwamhie tabia zako. Kuwa makini na marafiki unaochagua kuwa nao maishani.

23. Siku zote utavuna ulichopanda. Ukiona unapata matokeo ambayo huyataki kabisa basi jua kwamba umepanda kitu ambacho sio sahihi. Ili update matokeo ya tofauti unapaswa kupanda mbegu bora.

24. Maisha yana pande mbili ambazo zipo wakati wote. Huwezo kuzungumzia juu ukasahau chini. Huwezi kuzungumzia kulia bila kushoto, huwezi pia ukazungumzia uzuri bila ubaya. Utakapozungumzia mafanikio lazima pia utaongelea kujifunza. Kwa hiyo mzizi wa mafanikio ni kujifunza.

25. Unapaswa kuwa ndoto kubwa na kitu cha kukusukuma wewe kila siku. Kuwa na kitu ambacho kitakuamusha asubuhi na mapema  na kufanyia kazi. Unapaswq kuwa na kusudi lako LA maisha.
Ndoto kubwa na malengo makubwa sana

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X