Mara kwa mara ukiskiliza vyombo vya habari utagundua kwamba waafrika walio wengi wanahama na kusafiri kwenda nje ya bara la afrika na haswa ulaya ili kutafuta fursa. Wakati huohuo watu ambao sisi tunawaita wawekezaji wanatoka ulaya kuja Afrika kutafuta fursa pia.
Sasa labda swali linabaki fursa zipo wapi? Zipo ulaya au Afrika?
Je, wote tuhame twende ulaya kutafuta fursa?
Leo hii nimekuandalia mambo machache kuhusu fursa ambayo ningependa uyafamu. Kabla sijaanza kukueleza mambo haya naomba kama bado hujajiunga na mfumo wetu wa kutokea Makala kwa email BONYEZA HAPA ili usipitwe.
Moja, fursa zipo kila sehemu. Ni wajibu wako kuangalia kwa jicho la kipekee namna gani unaweza kukamata fursa na kusongambele.
Pili, fursa ni kama daladla ikikupita moja nyuma inakuwepo nyingine ambayo inafuata.
Tatu, sehemu yenye matatizo mengi ndio sehemu yenye fursa kubwa. Afrika kuna matatizo mengi, hivyo fursa za kibiashara ni kubwa afrika kuliko ulaya
Nne, usikimbizane na kila fursa. Uwe makini na fursa ambazo utaamua kufanya na zipi utaachana nazo, yaani ambazo hutafanya. Sio kila fursa inakufaa