Moyo wako Uko wapi?


“Fanya unachopenda” ni usemi ambao umekuwa unatumiwa kuwashauri watu  ili waweze kufanya kitu cha kitofauti na kipekee sana.
Jambo hili ni la kweli ndio maana siku ya leo ningependa kutilia mkazo na kusisitiza kitu hiki kwa herufi kubwa.

Watu wengi waliofanya makubwa katika sekta zao ni wale ambao walikuwa wanapenda kile wanachofanya. Na walikifanya kwa moyo na kujitoa.

Ukifanya kitu kwa moyo na upendo wako wote utaweza kukifanya kwa viwango vikubwa. Steve Jobs alikuwa na mapenzi na kompyuta, alijituma na alihakikisha anafanya kitu cha tofauti katika kila kitu ambacho alifanya.

Unajua kwa nini alikuwa anafanya hivi? Kwa sababu alikuwa anapenda kile anachofanya. Inawezekana Jobs alikuwa hahisi kama vile anafanya kazi. Mtu mmoja amewahi kusema kwamba unapofanya kile unapenda hutahisi kama kufanya kazi.

Inashauriwa kama Sasa hivi upo eneo ambalo halikufurahisi basi utapaswa kufanya mambo mawili,
1. Kuachana na unachofanya na kuanza kufanya kitu kingine unachopenda au
2. Kupenda unachofanya na kukifanya kwa bidii na moyo wote.

Kazi ya kufanya leo. Jiulize Je, kwa sasa ninafanya kile ninachopenda?

Pili jiulize ni kitu gani ninapenda kufanya?

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA
Hakikisha umesubscribe kwenye YouTube Channel Yangu Ya Youtube Kwa Kubonyeza Hapa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X