Namna Watu Wa Kawaida Wanavyofanya Mambo Yasiyo Ya Kawaida


Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii njema sana ya leo. Kila siku inayokuja kwako imebeba baraka, hivyo hakikisha kwamba unaitumia vyema kufanya makubwa. Siku hii ya leo napenda tuongee laa undani na kuona ni kwa namna gani watu wa kawaida wanaweza kufanya mambo ambayo sio ya kawaida.

Watu wote ambao tunawaona wameweza kufanya mambo ambayo sio ya kawaida walikuwa wa kawaida katika jamii kama hizi tunazoishi sisi. Ni watu ambao wamevuta pumzi kama ambayo tumevuta sisi na ni watu ambao wamekutana na changamoto, pengine changamoto zao ni kubwa sana kuliko changamoto ambazo sisi tunakutana nazo. Ila watu hawa hawakukata tamaa, ndio maana leo hii wewe unawashangilia na kuyaona mafanikio yao kama vile sio kitu cha kawaida. 

Kuna namna ambayo watu wa kawaida wanaitumia kufanya mambo ambayo sio ya kawaida. Na namna hii ndio ningependa kukushirikisha siku hii ya leo. Kama na wewe unapenda kushiriki kufanya mambo ambayo sio ya kawaida basi tafadhali sana Fanya yafuatayo.

1. Tafuta kitu kimoja au ndoto moja ambayo utasema hata iweje, mimi nitakufa na ndoto hii. Nitafanya na kuitimiza asubuhi, mchana na jioni bila kuchoka siku zote saba za wiki januari mpaka disemba mpaka kieleweke.

2. Kubali kuonekana kilaza na mwehu. Watu wengi waliofanya mambo ambayo sio ya kawaida ni watu ambao walikubali kufanya mambo ambayo yaliwapunguzia sifa zao. Kuna wakati walikuwa wanaonekana kama vilaza, watu wasiojielewa na watu ambao jamii iliona wamekuwa vichaa. Ila wao kwa sababu walikuwa wanasukumwa na ndoto kubwa. Kubwa kuliko maneno ya watu, waliweza kusonga mbele bila kukata tamaa.

3. Kubali kuchekwa. Kutokana na kwamba watu hawa walikuwa na ndoto kubwa sana, hivyo watu hawa walikuwa wanafanya vitu ambavyo havikuwahi kuonekana ni vya kawaida. Na walikuwa wanaongea mambo makubwa kiasi kwamba wanaonekana kama wamekeungeuka. Watu waliwacheka sana. Ila hawakukata tamaa, walisonga mbele na kuhakikisha kwamba hakuna kitu ambacho kinawakwamisha kufikia mambo makubwa.

4. Kumbatia matatizo.
Watu hawa ni watu ambao wamepitia katika matatizo makubwa, ila kwao matatizo hayakuwa tatizo. Bali matatizo yamekuwa dataja la wao kusonga mbele. Walijua wazi kabisa kwamba hakuna watu ambao hawana matatizo kabisa. Hivyo kwako ilikuwa ni au wabadilishe matatizo kuwa daraja la kusongambele au wayafanye matatizo kuwa fursa.

5. Soma Vitabu. Niambie mtu yeyote ambaye amefanikiwa ili nikwambie vitabu anavyosoma. 
Kiukweli mpaka leo hii sijakutana na mtu mwenye mafanikio makubwa ambaye hasomi vitabu. Utakuta watu hawa wanajichimbia na kusoma vitabu na vitabu . Kwenye nyumba zao wana maktaba kubwa sana za vitabu ambazo wanazitumia mara kwa mara. 
Wanasoma Vitabu ili waweze kupata mwanga wa kusonga mbele. Wanasoma Vitabu kupata mawazo mapya ya biashara.
Wanasoma Vitabu ili kuboresha kile ambacho walikuwa wanafanya. 
6. kuipa muda ndoto yao. hiki ni kitu kingine cha kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa. hawana papara ya kukimbilia mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi. wanaamua kuiipa muda ndoto  yao huku wakiifanyia kazi hata kwa kutokea chini.
SOMA ZAIDI: Huyu Ndiye ARNOLD SHWARZENEGER Na Mambo Matano Ya Kujifunza Kutoka Kwake

Hii ndio siri ambayo watu wanaofanya mambo yasiyo ya kawaida wanaitumia. Kumbuka kwamba watu hawa ni watu wa kawaida kama wewe ila wanaweza kufanya mambo ambayo sio ya kawaida kwa kutumia kanuni na mbinu ambazo tumeziona hapo.

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X