Hivi kama wewe ndio mteja na hiyo biashara unayofanya Sasa hivi inamilikiwa na mtu mwingine ungeenda kweli kununua hapo? Je, kitu gani kingekufanya ukanunue. Je, kama wewe ungekuwa mwajiri na na kazi unaoifanya inafanywa na mtu mwingine. Je, ungeendelea kumbakiza kwa utendaji huo? Kwa nini?
Hivi kama wewe ungekuwa tayari umefikia ndoto zako zoote za maisha ungefanyaje? Je, ungekuwa unafanya unachofanya sasa hivi?
Je, kama wewe ungekuwa ndiwe mtu bora zaidi katika kazi unayofanya Sasa hivi duniani, ungekuwa unafanya nini?
Hili ni swali muhimu sana kujiuliza rafiki yangu. Linakupa majibu ambayo kama utayafanyia kazi basi hutabaki kama ulivyokuwa hapo awali. Badala yake unapiga hatua. Kwa hiyo mara kwa mara jiulize. Ningekuwa Mimi ningefanyaje?
Kama utapata jibu ambalo linakuhitaji urekebishe. Rekebisha mara moja ili uweze kusonga mbele.
Asante sana.