Tafiti zinaonesha kwamba ni asilimia moja tu ya watu duniani ndio wanaofurahia mazuri na kumiliki asilimia kubwa sana ya uchumi. Ni asilimia moja tu ya watu ambao huwa wanafikia ndoto zao maishani huku wengine wakiishia njiani.
Watu huacha kufuatilia ndoto zao kwa sababu wakatikufuatilia ndoto zako ni sawa na kuamua kujitupa kwenye maji ili kuogelea. Waogeleaji wengi huishia kati kati kwa sababu huwa hawaoni alama ya kumalizia iko wapi. Yaani wewe hupaswi kuacha kwa sababu umekutana na changamoto na hivyo kuifanya alama ya kumaliza iwe mbali sana. Kama alama hii haionekani, haimaanishi kwamba sasa huo ndio wa mbio. Na wala haimaanishi kwamba hautafika
Sasa hapa kuna hasara tano ambazo zitajitokeza endapo wewe hapo utaacha kufuatilia ndoto zako.
1. utafanya mambo yaonekane ni magumu zaidi ya yalivyo. Ni ukweli kwamba mambo ni magumu. Ila sio kwa kiwango kikubwa kama ambavyo unataka kuuonesha ulimwengu.
Kwa hiyo utapaswa kusonga mbele. Ushindi huwa haupatikani kwa kuacha kufanya kitu bali kwa kusonga mbele na safari mpaka mwisho wa safari.
2. utapoteza muda wako, pesa na nguvu zako
Pale unapoanza kufanya kitu lazima kuna utawekeza kitu kwenye kutimiza ndoto zako. Utwekeza muda, utwekeza nguvu, utawekeza pesa na vitu vingi. Sasa kama ukiishia njiani utakuwa umeamua kupoteza vitu vyote hivi kabla hujafikia mwisho kabisa.
Hata kam utasema kwamba mbona nilikuwa sijaweka pesa sana hapa. Ila ukweli ni kwamba muda wako ni pesa pia. Kama usemi wa kiingereza unavyotuasa kwamba muda ni pesa au muda ni mali.
Ngoja nikwambie kitu kukhusu vikwazo na matatizo na changamoto utakazokutana nazo njiani. Unapokuwa umeweza kutatua changamoto hizi, ukweli ni kwamba hata hukumbuki kwamba umeshapitia kwenye changamoto kama hizo hapo. Utakachokuwa unaona machoni kwako ni ushindi ambao tayari unao mbele yako.
3. Utawanyima wengine hamasa ya kusoga mbele. Kuna watu wanakuangalia wewe hapo kama mfano wa kuiga maishani mwako. Inawezekana sio wengi sana ila wapo. Sasa ukiamua kuishia njiani. Maana yake utakuwa umeamua kuwakatisha tamaa hawa hapa ili waone kwamba maisha ni magumu na ni vigumu kufanya maajabu maishani mwao.
Hivyo basi usikubali kabisaa kuipoteza ndoto yako na kishia njiani.
Jipatie nakala ya kitabu cha Jinsi ya kufikia ndoto zako ili uweze kujifunza mengi kuhusu ndoto yako sasa. tuwasiliane kwa 0755848391