Huyu Ndiye ARNOLD SHWARZENEGER Na Mambo Matano Ya Kujifunza Kutoka Kwake


cover
Moja kati ya watu ambao dunia inawafahamu kwa kufanya makubwa basi ni mwigizaji wa mjengaji wa viungo vya mwili (body builder) Arnold Schwarzenegger.
Huyu akiwa mtoto, wazazi wake walimpeleka ili akajifunze mpira wa miguu. Alikuwa anaenda kila siku na kufanya mazoezi kama wengine wanavyofanya ila kwake hicho hakikuwahi kuwa kitu ambacho kinamsukuma zaidi. Kila mara alihisi kama kuna kitu ambacho hakijakaa sawa ila hakujua hicho kitakuwa ni kitu gani. Siku moja mwalimu wake wa mpira alimwambia Anord na  wanafunzi wengine wa mpira wa miguu wawe wanaenda kufanya mazoezi ya kunyanyua vyuma kila siku kabla ya kuanza kucheza mpira. Siku Arnold alipoanza kunyanyua vyuma, ndio aliona kile kitu ambacho alikuwa anakitafuta kila siku sasa ndio amekipatia jibu. Kile kitu ambacho kilikuwa hakijakaa sawa, sasa ndio alijua ni kitu gani hicho. Aliona kwamba eneo ambalo alipaswa kuwa ni  hapo kwenye kunanyua vyuma na wala sio sehemu nyingine.
Kuanzia siku hiyo akaachana na kucheza mpira wa miguu na kuanza kufanya mazoezi ya kujenga mwili.  
Ikawa katika usoma magazeti Arnold alikutana na hadithi ya Reg Park. Huyu alikuwa njenga viungo wa uingereza ambaye alishinda tuzo ya mr. universe na baadae kuingia kwenye tasnia ya uigizaji. Alifanya vizuri huko na kupata hela ambazo alizitumia kujenga eneo zuri la kufanyia mazoezi.
Tayari Arnold alikuwa na mtu wa kumwangalia. Tayari alikuwa na ndoto. Alitaka kuwa kama Reg Park.
Lakini sasa kuna tatizo ambalo lilijitokeza. Watu hawakuelewa  ndoto yake. Wazazi wenyewe hawakumwelewa. Hata baada ya yeye kushinda tuzo yake ya kwanza ya Mr. universe, wazazi wake hawakumwelewa.
Alijituma na hatimaye kupata tuzo ya m r. universe na baadae kupata  tuzo za mr. olypia mara tatu mfululizo.
Hii ndio kusema kwamba kama Anord angeendelea na uchezaji wa mpira basi huyu tunayemjua leo asingekuwa ni yeye bali mtu mwingine.

cover
Sasa kuna mambo manne ambayo tunaenda kujifunza kutoka kwa Arnold
1. Kuwa na ndoto na maono ya kufanyia kazi maishani mwako.
Arnold anasema kwamba ndoto na maono ndivyo vinakuelekeza wapi unapaswa kuwenda wapi. Vinakuonesha njia sahihi ya kufuata ili kuweza kufika huko. Anaendelea kusema hivi  unaweza kuwa na meli bora sana na ukawa na nahodha wazuri kuliko wote duniani  ila kama haujui unaelekea wapi ujue utazunguka huku na huko na mwisho wa siku hautafika sehemu ya maana
2.Kamwe usifikiri kwa udogo
Arnold anasema kwamba siku zote lenga kupata nyota. Na kinachowafanya watu wasifikirie kuwa na ndoto kubwa ni kwa sababu tu ya kuogopa kushindwa. Unachopaswa kufahamu ni kwamba kama hauna ndoto kubwa tayari umeshashindwa.
Yeye kwenye maisha amekuwa anaweka ndoto kubwa na ambazo mpaka sasa hivi amezifikia kwa viwango vikubwa sana.  Alikuwa na ndoto ya kuwa body builder mkubwa na aliweza kuifikia na kupata tuzo nyingi kwenye hilo eneo.
Alikkuwa na ndoto ya kuwa mwigizaji anayelipwa sana. Ameweza kufanikisha hilo pia kwa viwango vikubwa.
Alikuwa na ndoto na kuwa kwenye nafasi kubwa kisiasa. Ndoto hiyo iliweza kufikiwa kwa yeye kuwa gavana na jimbo la California nchini Marekani.
Anasisitiza mimi na wewe tuwe na ndoto kubwa kubwa.
Hapa ndipo naukumbuka tena ule usemi wa Donald Trump unaosema kwamba, katika maisha yako utapaswa kufikiri na kama utapaswa kufikiri kwa nini usifikiri kwa ukubwa zaidi?
3.Achana na wakatisha tamaa.
Arnold anasema kwamba katika maisha utakutana na watu ambapo wanakatisha tamaa..
Lakini  kamwe, usikubali wakatisha tama wakurudishe nyuma kwenye maisha yako Mtu akisema haiwezekani wewe sikia inawezekana.
Mtu akisema haijawahi kufanyika sikia inafanyika
Mtu akisema hapana unapaswa kufahamu kwamba hiyo ndio NDIO. Kuna usemi kutoka kwa Nelson Mandela ambao unasema kwamba siku zote huwa haiwezekani mpaka pale mtu anaposababisha kile kitu na kiwezekane. Unaweza kuweka rekodi mpya.
Arnold anasema kwamba laiti angewasikiliza watu basi ndoto zake zingeishia njiani. Alipotaka kuhamia marekani wakasema kwamba haiwezekani, aliposema kwamba anataka kuwa mjenga mwili mkubwa sana wakasema hayo yanafanyika Marekani wala sio kwao Austria.
4. kubali kuwekeza muda wa kutosha kabla ya kufikia ndoto yako.
Arnold anasema kwamba kufikia ndoto zako sio rahisi hata kidogo. Utapaswa kuweka juhudi na kutumia muda wako mwingi kufanya mazoezi na kufanya vile ambavyo watu wengine hawafanyi.
Mfano Arnold anasema kwamba kuna kipindi alikuwa anafanya mazoezi kwa masaa matano kila siku. Baada ya hapo anaingia darasani kujifunza kuigiza. Baada ya ya hapo anajifunza kiingereza.
Anasema kwamba aliyaweza haya yote kwa sababu alikuwa anapangilia ratiba yake vizuri na kuhakikisha kwamba haipiti sekunde.  
Arnold anashauri ulale masaa sita tu kila siku na masaa mengine 18 uyatumie kufanya kazi na kujinoa kwenye kitu ambacho unafanya. Kama unajihurumia kiukweli unaweza usiyaone mafanikio makubwa sana maishani mwako.
Pia anashauri usiache ratiba yako huru sana kiasi cha kukufanya upoteze muda wako mwingi. Hakikisha kila dakika inakuwa na kitu ambacho unafanya.
5. kubali kutoka jasho na damu kabla ya kufikia kilele cha mafanikio.
Arnord ni miongoni mwa wale watu wanaoamini usemi wa waziri mkuu wa uingereza Winston Churchill wa damu, jasho na machozi.
Na kwa hili hapa anatolea mfano wake kipindi akiwa anaigiza. Anasema kwamba kuna siku alitokwa na damu wakati anaendelea kuigiza kwenye magoti. Director akwambambia waishie hapo ili Arnord apate matibabu kwanza. Lakini yeye alisema kwamba anachotaka kuona ni kile kilichompeeleka hapo kimekamilika. Kwa hiyo waliendelea kurekodi  tamthiliya wakati yeye anatokwa na damu mpaka ikaisha.
Anasema kwamba kwenye maisha, nyakati kama hizi utakutana nazo sana. Lakini hupaswi kukata tama bali unapaswa kunyanyuka na kusonga mbele bila kukata tamaa.
Hayo ndio mambo matano ambayo tunajifunza kutoka kwa Arnold Schwarzenegger. Kwenye kitabu chetu cha mwezi wa 10 cha timiza ndoto zako tutakkutana na mengi zaidi kutoka kwa mtu huyu na magwiji wengine walio fikia ndoto zao.
Hakikisha unajiweka kwenye nafasi ya kupata kitabu hiki mapema sana kuanzia sasa. Utaweza kukipata kwa elfu mbili tu. Pesa hii unalipia kupitia nambari ya simu 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA.
Kwa kufanya hivyo utaunganishwa kwenye kundi la THINK BIG FOR AFRICA kwa mwezi mzima. Ambapo utakuwa unapata masomo mengine zaidi. Karibu sana.
KWA KUMALIZIA; mambo matano tunayojifunza kutoka kwa
1. kuwa na ndoto kubwa ambazo unazifanyia kazi
2. usifikiri kwa udogo
3. achana  na wakatisha tamaa
4. kubali kuwekeza muda wa kutosha kabla ya kufikia ndoto zako
5. kubali kutokwa jasho na damu kabla ya kufikia kwenye kilele cha mafanikio
Umekuwa name,
Godius Rweyongeza (songambele)
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com


One response to “Huyu Ndiye ARNOLD SHWARZENEGER Na Mambo Matano Ya Kujifunza Kutoka Kwake”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X