Mambo Muhimu Unayopaswa kuyafanya Unapoamka Asubuhii


Moja kati ya vitu ambavyo vimekuwa havielekezwi kwa umakini sana basi ni namna ya kuianza siku yako. Unapoamka asubuhi unakuwa na mambo mengi sana ya kufanya.
Wengi huutumia muda huu kufungulia redio na kusikiliza taarifa ya habari. Hata hivyo hapa napenda nikushirikishe namna sahihi ya kuianza siku yako.

Haupaswi kuianza siku yako kama mnyama au ndege. Kuna mambo machache ambayo ukiyafanya yatakunufaisha na kuifanya siku iwe ya kipekee. Hizi ni mbinu pia ambazo wataalamu na watu waliofikia mafanikio makubwa wamekuwa wanatumia.

Moja, jisemee maneno chanya
Kuna mtu ambaye ubora wa siku au ubaya wa siku unatokana na kile anachokutana nacho anapoamka. Akiamka akakuta mvua inanyesha basi anatoa tafsiri na kuiita siku hiyo njema au mbaya kulingana na anavyojisikia. Mwingine akisikia mlio wa mnyama fulani basi anatoa tafsiri kuonesha kwamba hiyo ni siku njema au mbaya. Ila nipende kusema kwamba  kila siku huwa ni bora. Ubora wa siku hautokani na hali ya hewa. Ubora wa siku unaanzia ndani yako. Anza kujisemea maneno chanya asubuhi unapoamka. Jisemee maneno chanya na maneno ya kukusukuma kufanya makubwa. Jisemee kwamba wewe ni mshindi, umezaliwa kushinda na utaishi kiushindi ndani ya siku hii mpya. Maneno mengine chanya unayoweza kujisemea ni kama……….

Pili, Soma malengo yako
Utumie muda huu wa asubuhi kuhakikisha unasoma malengo yako. Jiulize Je, bado ninatembea kwenye nia sahihi kuelekea ninapotaka kufika kimafanikio. Inashauriwa kila siku upate muda wa kupitia malengo yako walau mara mbili. Ila bado unaweza kupitia malengo yako zaidi ya hapo. Na muda mzuri wa wewe kupitia malengo yako ni asubuhi na mapema kabla hujakutana na uhalisia wa dunia.

Tatu pangilia ratiba ya siku nzima
Winston Churchill amewahi kunukuliwa akisema kwamba akipewa saa sita za kukata mti atatumia masaa manne kunoa panga na mawili kukata mti. Muda wako wa asubuhi ni mzuri kwako wewe kuanza kunoa panga. Unanoa panga kwa kupangilia nini utafanya. Baada ya hapa utaianza siku yako ukijua haswa ni nini unapaswa kutimiza.

Nne, soma kitabu, ianze siku yako kwa kusoma kitu chanya. Soma kitu ambacho kinakuongezea maarifa zaidi. Kumbuka kipato chako kitaongezeka mara dufu kama utaongeza maarifa yako mara tatu zaidi kama anavyotuasa Robin Sharma.

Tano, andika mambo ambayo kamwe hutafanya.
Mbali na kwamba umeshapangilia siku yako kwa kuandika nini utafanya. Andika pia yale ambayo hutafanya hata iweje.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X