“Get your face out of Facebook and get it into the book”
Unknown
Kama bado hujajiunga na mfumo wetu maalumu wa kutokea makala, bonyeza HAPA
Wiki Chache zilizopita nilikutana na usemi ambao nakubaliana nao kwa asilimia 100. Usemi huu mzuri
“unasema toa uso wako kwenye mtandao wa Facebook na uweke kwenye kitabu”.
Kiukweli huu ni usemi ambao haujaremba kitu.
Yaani kama unapenda kutengeneza maisha ya tofauti basi utapaswa kutoa uso wako Facebook na kuuweka kwenye kusoma vitabu kwa muda mwingi.
Ni ukweli kwamba Facebook na mitandao mingine inatuunganisha, lakini muda ambao watu wanatumia kwenye mitandao hii ni mwingi zaidi kuliko muda unaotumika kufanya kazi za kujenga. Imefikia hatua kila kitu ambacho mtu anafanya anakimbia kukiweka Facebook. Akiamka asubuhi basi anaweka Facebook
Akipata kifungua kinywa basi anaweka picha Facebook
Akikasirishwa bado na chenyewe anaandika Facebook. Kwa maisha ya sasa hivi unaweza kufuatilia maisha ya mtu Facebook na ukajua kila kitu alichofanya kwa siku nzima.
Sasa swali Je, haya yote yanakusaidia nini? Hivi ukiweka Picha kwamba upo hoteli fulani au umekutana na fulani inakuongezea thamani gani mishani mwako? Je, inaingiza pesa? Na Je, usipofanya hivyo utakufa?
Ubovu wa mitandao hii ni kwamba ukiangalia kitu facebook wanakuletea kingine kinachofanana na kile cha awali. Hivyo unajikuta unatumia muda mwingi kwenye ni mtandao huu kuliko muda unaoutumia sehemu nyingine.
Utafiti unaonesha kwamba watu wanaingia Facebook kila baada ya dakika tano mpaka kumi
Sasa umefika wa wewe kutoa uso wako Facebook na kuuweka uso wako kwenye Vitabu.
1. Soma kujiongezea Maarifa na kujitofautisha.
2. Ukisoma kitabu, utaimarisha Afya akili. Na Afya ya akili ambayo itapelekea kwako kuwa na Afya ya mwili na roho.
3. Soma ili kupanua fikra zako na kupata mawazo chanya ya kumujenga.
4. Soma pia kuongeza kumbukumbu na kupunguza kusahau sahau
5. Soma kukutana na watu ambao huwezi kukutana nao. Au ambao hata ukikutana na bado hutapata kila kitu kutoka kwao.
6. Soma ili kuongeza kipato chako😊.