Vitu Viwili Kuhusu Ndoto Ambavyo Watu Wa Kawaida Hawana (Kama Utakosa Vitu Hivi, Utaishia Kusikia Mafanikio Kwenye Vyombo Vya Habari).


Kama Utakosa Vitu Hivi, Utaishia Kusikia Mafanikio Kwenye Vyombo Vya Habari

Mwaka juzi wakati nasoma kitabu cha Who Will Cry When You Die nilikutana na kitu cha kushangaza kidogo ila ikabidi nikifanyie kazi. Mwandishi wa kitabu Robin Sharma alisahuri kwamba unapaswa kuwa na kitabu cha ndoto chenye orodha ya vitu 101 ambavyo utavifanyia kazi kabla ya kufa. Vitu hivi vinaweza kuwa ni ndoto, malengo na mipango yako ya muda mfupi na mrefu. Hiki ni kitu kimoja ambacho kina sehemh mbili

Kwa hiyo mpaka hapo tunaona vitu viwili muhimu vifuatavyo.
1. Unapaswa kuwa kitabu cha ndoto
2. Unapaswa kuwa na orodha ya vitu 101 ambavyo uyavifanyia kazi maishani mwako

Kabla hujaishia hapa ngoja tuendelee kidogo!

Ni watu gani ambao ungependa kukutana nao maishani mwako?

Sehemu gani ungependa kutembelea?

Lugha gani ungependa kujifunza?

Je, ungependa kuandika kitabu? Kitahusu nini? Mwaka gani?

Hivi kuna biashara au fursa unayiona kwenye akili yako? Ni ipi?

Gari gani ungependa kumiliki? Linafananaje? Nyumba je?

Je, unapenda kuwa huru kiuchumi? Itakuchukua nini na baada ya mwaka gani?

Afya yako je? Ungependa iweje?

Kama kuna kitu ungependa kufikia kati ya hivyo basi kiandike kwenye KITABU CHAKO CHA NDOTO.
Na hapo nimekupatia maswali ya kuanzia ili kutengeneza orodha ya vitu 101 ambavyo utafanyia kazi. Ni juu yako kuendelea mpaka ufikie 101.
Ngon nikwambie kitu.  Mimi mara ya kwanza niliandika vitu 21 tu. Rafiki yangu mmoja akaja akasoma hiyo orodha kisha akacheka. Akaniambia hivi, acha uoga. Andika vitu mpaka ufikie vitu 101. Nikagundua kweli ulikuwa uoga, nikaanza tena.

Sasa unajua nini?
Baada ya kuwa umefanya vitu vyote hivyo, kuna hatua saba hapa napenda uzifuate.
1. Orodhesha lengo au ndoto moja kubwa ambalo  utafikia maishani.

2. Weka sababu tano kwa nini utafikia lengo au ndoto hiyo. Katika nyakati ambazo utakutana na ugumu rudi kwenye KWA NINI zako ili zikupe moto za kusongambele katika kutimiza ndoto yako.

3. Chukua kalamu na karatasi na andika kila kitu ambacho kitahitajika kufikia ndoto hii. Andika kila hatua ambayo unafikiri utapitia kabla ya kufikia ndoto zako.

4. Andika vikwazo vyote ambavyo unafikiri vinaweza kujitokeza na hatua ambazo utachukua.

5. Andika majina ya watu muhimu kwako unayohitaji ili kufikia ndoto zako

6. Tengeneza orodha ya washauri. Hawa ni watu ambao watashiriki katika kukushauri na  kufikiri juu ya ndoto zako.

7. Eleza jinsi ya uyakavyojisikia endapo utafikia ndoto hii. Je, utakuwaje kiuchumi, kihisia, kiroho na mwonekano.

Huu ndio mwongozo wako wa kutengeneza orodha ya vitu 101 ambavyo utafikia maishani.
****************

🔥kama bado hujapata nakala ya kitabu cha jinsi ya kuibua ubunifu ulio ndani yako, chukua hatua leo. Kitabu kinapatikana kwa shilingi 7,000/- tu.
Tuma pesa kwenda 0755848391 jina Godius Rweyongeza.
Baada ya hapo nitumie ujumbe wenye barua pepe yako ili nikutumie kitabu.

Asante sana,

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X