Hivi Ndivyo Nilivyopata Bahati Ya Kukutana Na Donald Trump Na Mambo Matano Aliyoniambia


(kama unataka kuchomoka kwenye maisha basi utapaswa kuzingatia haya aliyosema)
Siku chache zilizopita nilikaa meza moja na raisi wa marekani katika maongezi mazito sana. Na katika maongezi haya alinishauri vitu vitano ambavyo ninaenda kuvidadavua hapa chini. Labda utakuwa unajiuliza huyu jamaa aliwezaje kukutana na raisi mkubwa hivyo. Ni rahisi sana na connection hii nimeitengeneza mwenyewe. Na wewe kama unataka nitakutengenezea connection hii ya kukutana naye bila kkuchelewa.
Nimekutana naye kwa kusoma kitabu chake cha How TO GET RICH. Katika kitabu ameniambia mambo yafuatayo.
Moja anasema kwamba  unapaswa kuwa unasukumwa na kitu zaidi ya pesa kwenye kufanya kazi zako za kila siku. Hiki ni kitu ambacho kitakufanya uweze kuongeza thamani zaidi na kuwafikiria wateja wako. Ila kama utasukumwa na pesa maana yake utakuwa unajifikiria wewe mwenyewe na namna ya kutengeneza faida  muda wote.  Hutaweka nguvu katika kutoa vitu ambavyo ni bora
Pili anasema kwamba  wakati wa maongezi yako au hat akama unaandika barua au ujumbe. Hakikisha kwamba ujumbe wako unakuwa ni mfupi na unaoeleweka. Usiwe mtu wa maneno mengi sana.
Tatu anasema kwamba unapaswa kuwa mkurugenzi wa maisha yako. Hivyo unapaswa kujua kwamba maisha ni wajibu wako, ukishinda ni juu yako lakini pia ukishindwa ni juu yako.
Nne, unapaswa kuhakikisha kamba unazungukwa na watu wanaoju. Kama unaajiri basi ajiri ambao wanajua. Usiajili tu ilimradi umeajiri. Kuwa na watu ambao muda wote ukitaka kujua kitu Fulani unaweza kuwauliza na wakakupa jibu sahihi.
Tano, usipoteze mwelekeo wakona wala usidanganywe na mafanikio ya muda mfupi. Trump anasema kwamba moja kati ya vitu ambavyo vilimwangusha sana ni yeye kupoteza mwelekeo kwa kile anachofanya. Hivyo anashauri kwamba unapaswa kuwa mtu wa kutopoteza mwelekeo wa maisha yake ili uweze kufikia hatua kubwa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X