Inalipa kutumia muda wako vizuri


Muda wako haupaswi kuutumia katika kufanya mambo ambayo haya kufai kabisa. Utumie muda wako kufanya kazi ambazo zinakuinua wewe na kuweza kukufikisha kwenye kilele cha mafanikio.
Pia jiwekee utaratibu wa kujikamata kila siku kuona kama leo umetumia muda wako vizuri zaidi. Unaweza kufanya hivyo kwa kupata muda wa kuitafakari siku yako kila siku  kabla ya kulala.
                   
Jiulize ni vitu gani umefanya vyema ndani ya siku ya leo. Je, ni vitu gani umefanya vibaya? Je, ni masomo gani ambayo umejifunza siku ya leo. Kama utaaweza kufanya hivi kila siku, ninahkuhakikishia hautaendelea kuwa mtu Yule Yule. Utaondokana na ule usemi ambao watu wengi wanautumia kwanba bora ya jana maana kwako kila siku mpya kwako itakuwa ni bora zaidi ya jana. Asante na nikutakie siku njema


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X