JE, WAJUA KWAMBA DAKIKA KUMI NA TANO ZINAWEZA KUKUFUNDISHA LUGHA MPYA? DAKIKA 15 MTANDAO NI ZINAKUPA NINI?


Kwa sasa hivi imekuwa kama kawida kwa watu kutumia muda mwingi mtandaoni wakiwa wanazurura huku na kule bila hata mwelekeao wa maana. Hata hivyo muda huu ambao wewe umekuwa unautumia mtandaoni unaweza kuanza kuutumia vizuri kuanzia leo hii ukajikuta kwamba umejifunza lugha mpya kwenye mtandao. Ni rahisi sana. Chagua lugha mpya ambayo  ambayo ungependa kujifunza. Kisha kwenye ule muda uliokuwa unautumia mtandaoni kila siku, toa dakika kumi na tano za kujifunza lugha mpya ambayo umechagua. Ukifanya hivi kwa mwaka mzima, wewe utakuwa tayari umekuwa mtu wa viwango vingine.

Nakutakia siku njema sana.

Godius Rweyongeza.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X