KITENDO KIMOJA, KIDOGO NA CHA UHAKIKA KITAKACHOKUWEKEZESHA KUWEKA AKIBA KWA VIWANGO VYA JUU SANA


Kuna utafiti nimewahi kusoma kwamba mwajiriwa mmoja kwa nchi za ulaya akiachishwa kazi siku hii ya leo anaweza kuendelea kuishi kwa siku nyingine zijazo 18 tu. yaani kwamba akiba yake aliyonayo kwa siku hii ya leo inaweza kumfanya aendelee kuishi kwa siku 18. Huu  ni utafiti unaonesha hali ya nchi za ulaya, sasa sijui hali ikoje kwako rafiki yangu. Je, wewe kama leo hii ungekuwa unaacha kazi au kama biashara yako ingekwama leo hii una uhakika wa kuendelea kuishi kwa siku ngapi zijazo? HIILI NI JIBU AMBALO NAJUA UNALO WEWE MWENYEWE TU.
Lengo langu leo hii nikukuonesha kitendo kidogo ambacho kinaweza kukufanya uweke akiba kubwa kwa viwango ambavyo hukuktegemea. Na kitendo hiki si kingine bali ni kitendo cha wewe kufungua akaunti yako benki kwa ajili ya kuweka akiba. Hivyo tu.
Ujue nini kitatokea pale ambapo wewe utafungua akunti yako benki. Ni kwamba akili yako itajua  kila mara inapopokea pesa inapaswa kutoa akiba kwanza kabla ya kitu kiingine. Na hivyo utalazimika kuweka pesa yako benki. Kwenye hiyo akaunti.
Kuna mataifa mawili ambayo kwa muda sasa yamekuwa yakitumia hii kanuni ya kufungua akaunti benki na kuweka akiba na yameweza kupiga hatua kubwa sana kiuchumi. Mataifa haya ni China na Israel. Wewe mwenyewe unaweza kuona ni kwa namna gani yanapamba moto kwenye sekta nyingi nyingi tu. sasa rafiki yangu, naomba nikusihi uchukue hatua mara moja na kwenda  benki kufungua akaunti ya kuweka akiba. Rafiki yangu huo ndio ushauri muhimu nilionao kwako kwa siku hii ya leo.

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X