Afrika yetu ina mambo mengi ambayo yanachukuliwa kawaida na watu ila ukiyaangalia kwa jicho la kusongambele, unaona wazi kwamba watu wanalazimisha kujweka vikwazo kwenye safari ya kutoka sifuri mpaka kileleni.
Moja ya vitu huvyo ni kauli ambazo zinazuia ubunifu na watu kusongambele. Kauli hizo ni pamoja na
1. Hakuna haraka barani Afrika
2. Ukitaka kumficha mwafrika kitu basi kiandike kwenye kitabu.
3. Mababu zetu hawakuwahi kufanya hivyo.
Japo kila kauli Kati ya hizo zote tatu ina madhara makubwa kwa maendeleo ya mtu binafsi. Kwa Leo napenda kuiongelea kiundani zaidi hiyo kauli ya tatu.
MABABU ZETU HAWAKUWAHI KUFANYA HIVYO.
Unakuta mtu ana wazo la kuboresha na kufanya kitu kwa namna ya tofauti, ila utasikia watu wanasema kwamba. Mababu zetu hawakuwahi kufanya hivyo. Yaani maana yake kitu kiendelee kufanyika kwa namna ile ile kilivyokuwa kinafanyika miaka 30 iliyopita. Hata Kama mtu atakuja na njia ya kuboresha na kufanya vizuri zaidi ila kama mbinu hiyo haikuwahi kutumiwa na mababu zetu Basi haifai.
Kama unavyoona kauli hii sio kauli ambayo inawafanya watu wachangamke. Hivyo basi sio kauli ya kuendekeza.
Kama ulikuwa unatumia kauli hii achana nayo mara moja, maana mambo yanabadilika. Kitu kilichowapa matokeo ya mazuri mababu zetu sio kitakacholeta matokeo makubwa sasa hivi. Zama zimebadilika.
Kauli hii pia inaua ubunifu. Watu wenye vipaji vyao wanakwama kuvitumia kwa sababu tu wanaambiwa mababu zetu hawakuwahi kufanya hivyo.
Kuanzia leo hii achana na kauli hii mbovu kabisa. Unachopaswa kufahamu ni kuwa, kama mababu zetu hawakuwahi kufanya hivyo basi wewe unaweza kuja na njia bora zaidi hata ya ile wakiyokuwa wanaitumia.
Bila shaka utakuwa unaona jinsi kauli hii inapaswa kuondolewa kwenye kamusi ya maongezi barani. Na wewe ndiwe unapaswa kuwa mstari wa mbele kufanya hivyo.
Makala hii imeandaliwa na
Godius Rweyongeza.
Godius Rweyongeza ni mwanzilishi wa mtandao wa SONGAMBELE (www.songambeleblog.blogspot.com) na programu ya THINK BIG FOR AFRICA.
Ukijiunga na programu hii utapata kitabu kimoja cha kiswahili kila mwezi pamoja na masomo ambayo huwezi kuyapata popote kila siku. Gharama ya kujiunga ni elfu 2 kila mwezi ambapo kwa kuanzia utalipia 10,000 ambayo ni gharama ya miezi mitano. Utalipia kwa namba 0755848391 jina Godius Rweyongeza Kisha utatuma ujumbe ili uungwe kwenye kundi la WhatsApp programu inapoendelea.
Karibu sana.
Kupata makala maalum kila wiki BONYEZA HAPA