WALE MNAOSEMA KILA KITU KINA FAIDA NA HASARA, EBU NIAMBIE FAIDA ZA KUWA MASIKINI!!!


Imezoeleka miongoni mwa watu kwamba kila kitu huwa kina pande mbili. Ukizungumzia kulia huwezi kusahau kushoto. Ukizungumzia mbele basi lazima kutakuwa na nyuma.  Ukisikia mtu anasema juu Basi lazima kuna chini.

Moja ya kitu ambacho watu wamezoea kusambaza ni kwamba kila chenye faida basi lazima kitakuwa na hasara. Japo kitu hiki kinafanya kazi katika baadhi ya maeneo lakini kwenye suala la utajiri na umasikini basi sioni faida za kuwa masikini.

 Inawezekana wewe ni mdau wa hiyo kauli ya kwamba kila chenye faida  basi lazima kitakuwa na hasara. Sasa ebu niambie faida za kuwa masikini ni zipi?

Kitu kikubwa ninachoona ni kwamba,
👉ukiwa masikini utashindwa kulipa kodi muhimu

👉utashindwa kupata huduma muhimu ambazo unastahili

👉utashindwa kupata huduma bora za kiafya

👉 Utashindwa hata kusomesha watoto wako au hata wewe mweyewe kujiendeleza kielimu..

👉utajificha ili usionekane hata kwa watu hasa kama unadaiwa.

soma zaidi; inawezekana kuondokana na madeni

👉utashindwa kutoa sadaka kadiri ya imani yako.

👉👉na kuendelea na kuendelea

Orodha ya hasara za kuwa masikini ni nyingi sana.
Zikitajwa zote hapa Basi kitakuwa kitabu cha aina yake.

Kiufupi faida za umasikini ni HAMNA labda Kama wewe unazijua niambie.

Hivyo basi kuanzia sasa jihakikishie unajifunza misingi ya fedha na kuiishi.

Hakikisha unakuwa na malengo ya kutafuata.

Fanya kazi na toa thamani ili upate fedha zaidi.

Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.
Godius Rweyongeza
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X