Hivi Ndivyo Utaweza Kujifunza Lugha Mpya 2020 (Ukiamua kuitumia vizuri njia hii, mwakani watakusikia ukinena kwa lugha nyingine)


Inawezekana umekuwa na mpango wa kujifunza lugha mpya kwa siku sasa, ila Kuna vitu vinakuzuia.
1). Pengine unaona gharama za kuingia darasani ni kubwa.
2). Majukumu yako ni mengi kiasi kwamba unaona huwezi kuyaacha kuanza kuhudhuria darasa jipya.
3). Hujui wapi unapaswa kwenda kujifunza lugha mpya.
Sasa leo hii napenda nikwambie wapi utaweza kujifunza lugha mpya 2020.  Njia hii ni kutumia app inayoitwa DUOLINGO.
  •   Njia hii haihitahitaji muda mwingi kutoka kwako. Yaani utahitaji dakika tano mpaka 15 kila siku.

Na huu Ni muda ambao naamini kabisa huwezi kuukosa. Najua huu ndio muda ambao huwa unautumia ukiwa mitandaoni. Najua huu ndio muda ambao huwa unautumia kuangalia tamthiliya. Ila zamu hii tutaufanya uwe wenye manufaa kwako. Kwa muda huu utajifunza lugha mpya

  •   Njia hii pia haitahitaji gharama. Gharama kubwa utakayotumia ni kuhakikisha una kifurushi.

Hiki najua sio shida kwako Kama umeweza kusoma hapa leo.

  • Kwa njia hii utaweza kujifunza   ukiwa nyumbani kwako, ofisini au hata safarini.

Ninaamini kwa mwaka ujao, hutakosa hata siku moja ya kujifunza maana unaweza kujifunza ukiwa popote.
TUONGEE KIDOGO KUHUSU DUOLINGO.
Hii app unaweza kuipakua kwenye simu yako kutoka kwenye playstore au appstore. Ukishaipakua utaamua ni lugha gani unapenda kujifunza na utaanza Mara moja bila kuchelewa.
Bila shaka unaona jinsi ilivyo rahisi.
KITU KIMOJA KINACHOHUTAJIKA KUTOKA KWAKO KABLA HUJAPAKUA DUOLINGO.
Ukiwa na Duolingo utaweza kuchagua lugha yoyote unavyopenda kujifunza. Lakini utapaswa kuwa unajua walau lugha ya KIINGEREZA.
Hiki ni kitu kimoja na pekee kinachohitajika kutoka kwako.
Naamini baada ya hapa utaenda kupakua app hii ya DUOLINGO kwenye simu yako
Nitafurahi Kama utaniambia wewe unaenda kujifunza lugha gani 2020. Asante sana,
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Unaweza kuwasiliana na mwandishi kupitia namba 0755848391
 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X