JE, TUJIFUNZE NINI KUTOKANA NA UZINDUZI WA CYBERTRUCK?


Masomo matano ya kibiashara kutoka kwa Elon Musk na Kampuni yake ya Tesla

  Ni mwezi sasa umepita tangu Elon amezindua gari aina ya Cbyertruck ambayo imetegenezwa na kampuni yake ya Tesla. Cbertruck ni truck (pick up) ya kipekee tofauti na pickup za magari mengine ambazo umezoea kwa siku zote. Yaani Tesla wamekaa chini na kuja muundo  mpya kabisa .

Siku ile ya uzinduzi watu walichanganyikiwa, maana aina ya gari waliloona linaingia ukumbini halikuwa sawa na lile ambalo wao walikuwa wanategemea kuona. Watu walidhani hiyo truck itakuwa ni sawa na pickup za makampuni mengine kama Ford na Toyota.
Gari hilo ambalo halipitishi risasi (bulletproof) lilipigwa                      na nyundo siku ya maonesho na wala halikuonesha dalili zozote au alama yoyote  ya kukwanguliwa. Hata hivyo viooo vyake vilivunjika wakati wa maonesho baada ya kurushiwa chuma. Na hiki kilikuwa ni kinyume na watu walivyokuwa wanategemea.  Maana vioo vya gari pia ilitegemewa visikwanguliwe hata kidogo hata baada ya kurushiwa chuma.

Baada ya uzinduzi w gari hilo kumekuwa na majadiliano makubwa kwenye mitandao ya kijamii. Sasa hivi ukiiiingia google na kuandika tesla cbyertruck unapata matokeo 46, 800,000. Hahah, milioni arobaini na sita laki nane!!!  Sasa leo hii ningependa tuongelee masomo muhimu ya kibiashara ambayo tunaweza kujifunza kutokana na uzinduzi huu wa gari hili la Tesla.

MOJA, UKITENGENEZA KITU CHA KIPEKEE WATU WATAKIONGELEA TU
Kama nilivyokwambia kwamba gari hili linaongelewa sana kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii.
Wapo watu ambao wameonekana kupenda sana muundo huu mpya wa gari hili la Tesla, wakati wengine wakionekana kuwa hawajapenda. Mashirika mbali mbali yameonekana yakicchukua gari  hilo na kuweka logo zao na kuzitupia mtandaoni, kitu cha kipekee kinachofanya gari iongelewe zaidi ni swali ambalo watu wanajiuliza, kwanini vioo vya gari vilivunjika baada ya kurushiwa chuma?

Somo kubwa la kibiashara ambalo napenda ujifunze kutokana na uzinduzi huu wa gari hili ni kuwa unapotengeneza kitu cha kipee basi watu lazima watakiongelea tu.

Kwenye ulimwengu wa magari hakujatokea mabadiliko makubwa sana ya pickup tangu miaka ya Henry Ford. Karibia miundo inayotumika sasa hivi ni ile ile iliyokuwa inatumika miaka hiyo ya Henry Ford. Ila sasa Elon Musk amekuja na kitu cha kipekee. Na hivyo lazima watu wakiongelee.

Elon Musk angeweza kutumia muundo ule ule kama wa pickup za kampuni megine kwa  kuweka mfumo wa umeme ndani yake tu. ila amekaa chini na kutengeneza kitu kipya kabisa ambacho ulimwengu haujawahi kuona.

PILI, WATU WAKIONA KITU MARA YA KWANZA WATAKIKATAA, ILA WAKIJIHOJI TENA WATAONA NI KITU AMBACHO HAKIKWEPEKI
Akili ya binadamu huwa inakuwa ngumu kupokea vitu vipya vinapotolewa. Na hili linaturudisha nyuma kidogo mpaka mwaka 2007, ilipozinduliwa iphone ya kwanza. Watu mwanzoni walionekana kuikataa maana ilikuwa imeenda kinyume na matarajio ya wengi. Wengi walikuwa tayari wamezoea simu zenye kibodi lakini sio hizo za ku pangusa na kidole.

Lakini simu zilivyoingia sokoni kila mmoja akawa anahitaji moja ya wake.

Sasa kitu hiki ndio nakiona kwa gari hii aina ya cybertruck ya Tesla. Siku ya uzinduzi ilionekana kama kituko kwa wengi ila sasa kila mmoja anakimbia kuweka oda yake ili awe miongoni mwa watu wa kwanza kupata hilo gari litakapotolewa.

Elon musk mwenyewe anasema hilo ndilo gari ambalo litatumika siku zijazo.

TATU, UNAPOAMUA KUFANYA KITU, USIIBE WATEJA. TENGENEZA SOKO JIPYA KABISA
Kwa kitu alilchofanya Elon Musk sio kwamba anaenda kuiba wateja kidogo kutoka kwenye makampuni ya magari yaliyopo sasa hivi. Ila ametengeneza soko jipya kabisa ambalo halijawahi kuwepo.

NNE, UKITENGENEZA KITU BORA ZAIDI WATU WATAKUSAIDIA KUTANGZA.
Mpaka sasa hivi Elon Musk hajatoa hata senti moja kulitangaza gari lake kwa watu, ila watu wengi wanakimbilia kuweka oda. Hii inatoa picha ni kwa namna gani watu wanavyoshirikiana kutangaza hilo gari lake kwa wengine.

TANO, UNAPOWAACHIA WATU NAFASI YA KUONGEA, UNAPATA KUJUA MENGI
Baada ya vioo vya dirisha kupasuka kwenye maonesho. Sasa kila mmoja anajaribu k utafuta kwa nini vilipasuka. Gazeti la Forbes limeandika sababu kumi za kwa nini vioo hivyo vilipasuka. Hii ni kuonesha ni kwa namna gani watu wapo tayari kujieleza na jinsi unavyoweza kujifunza zaidi kutoka kw hawa watu.

Elon Musk amewaachia watu nafasi ya kujieleza nina hakika maelezo haya ya watu anaenda kuyafanyia watu ili kuja na kitu kingine ambacho kitakuwa ni bora zaidi ya hapa.

Rafiki yangu hayo ndio masomo matano ya kibiashara ya kujifunza kutokana na uzinduzi wa gari hii mpya aina ya cybertruck ilizinduliwa na kampuni ya Tesla mwezi uliopita.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Unaweza kuwasiliana na mwandishi kupitia barua pepe ya songambele.smb@gmail.com
Unaweza pia kuwasiliana naye kupitia wasapu namba 0755848391 karibu sana.

JIUNGE NA KUNDI LA THINK BIG FOR AFRICA LEO ILI UWEZE UKUJIFUNZA ZAIDI KUPITIA KUNDI HILO
Gharama ya kujiunga na kundi ni 2000 tu kwa kila mwezi ambapo utaendelea kupata masomo kila siku na kitabu kimoja cha kiswahli kila mwezi. Utalipia hiyo gharama kupitia nambari ya simu ambayo ni 0755848391 jina ni Godius Rweyongeza. Baada ya kufanya malipo utanitumia ujumbe mfupi kupitia hiyo hiyo namba ili niweze kukuunga kwenye kundi. Karibu sana


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X