Kutana na mtu mwenye kumbukumbu kali kuliko wote


Kuna kipindi nilikuwa nasoma vitabu vya namna bora ya kuwa kumbukumbu ambavyo vimeandikwa na mwandishi Harry Lorrayne na waandishi wengine. Nilichojifunza kwenye vitabu hivi Ni kuwa unaweza kuwa mtu mwenye kumbukumbu kadri unavyotaka.
Una uwezo wa kukumbuka namba za simu za watu, una uwezo wa kukumbuka namba yenye urefu mpaka namba 21 na zaidi.
Una uwezo wa kukumbuka majina ya watu unaokutana nao. Una uwezo wa kukumbuka tarehe na bila kutembea na kalenda.

Kwa mfano nikikuuliza tarehe 17 machi 2020 itakuwa siku gani? Kwa kutumia mbinu hizo una uwezo wa kusema siku hiyo lakini hata siku za miaka ya nyuma  hata Kama ni mwaka 1901. Kuna kanuni ndogo tu za kutumia na ukafanikisha hili.

Hata hivyo lengo langu kwa siku ya leo halikuwa kutaka kukuonesha uwezo wako wa kumbukumbu ulionao. Nataka nikwambie mtu mwenye kumbukumbu kuliko wote. Huwezi amini mbali na uwezo ambao nimesema kwamba wewe unaweza kuwa nao Kama utaamua. Kuna mtu mmoja anakuzidi kwa uwezo wa kumbukumbu na huwa hasau hata kidogo. Mtu huyu ni yule anayekudai.

Kama unadaiwa usitegemee hata siku moja kwamba anayekudai atasahau. Nimekuja kugundua kuwa watu pekee wenye kumbukumbu za kimataifa ni wale ambao wanadai. Hata iweje lazima atakumbuka kwamba mtu fulani namdai kiasi fulani na inanipasa nimtafute anilipe.

Hivyo basi nipende kukusihi kwamba namna Bora ya kuwakwepa watu wa namna hii daima ni kuhakikisha kwamba hudaiwi. Au kiufupi ni kwamba usijikopeshe.

Ila UKIFANYA hivyo kwa mategemeo kwamba watawasahau. Nakuhakikishia kitu kimoja. Watu hawa hawasahau.

Hivyo njia ya kujipa wewe uhuru wa kutosumbuliwa ni kuachana na kukopa

Kwa Leo naishia hapo, naomba nikutakie wakati mwema.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Unaweza kuwasiliana naye kwa nambari ya simu 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X