Kwenye dunia hii kila mmoja ana jukurmu lake. Kuna watu ambao jukumu lao ni kukosoa, kukatisha tamaa, na kukukwamisha. Hawa watu utakutana nao katika safari yako. Ila kumbuka kwamba wao kazi yao waliyoichagua ni kukosoa.
Ukiona mtu anakukosoa na kusema vibaya juu ya kile unachofanya, Jua kwamba yeye amechagua hiyo kazi. Hivyo wewe endelea na shughuli zako bila kujali anachosema.
Kikubwa wewe kila mmoja atimiza majukumu take vizuri. Na wewe jukumu lako kubwa ni kuweka njia ili wengine waweze kufuata.
Nakutakia siku njema sana.
One response to “Nakukumbusha Jukumu Lako Hiki Usije Ukasahau”
Ahsante sana kwa ujumbe mzuri wenye busaraa